UFUNUO 1:3-4,20 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na
kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Yohana, kwa yale
makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye
aliyeko na Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na
ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa
saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
KANISA LA KWANZA LA EFESO;
I.
JE MAKANISA SABA YANAMAANISHA NINI?
MAANA YA KWANZA YA MAKANISA SABA- Majina
ya makanisa Saba ni mfano wa kanisa katika zama mbalimbali za kikristo
MAANA YA PILI YA MAKANISA SABA-Ni mifano iliyotumiwa
huonyesha hali ya kanisa Kwa nyakati tofauti katika historia ya ulimwengu.
MAANA YA TATU YA MAKANISA SABA- Makanisa saba
yanasimama badala ya kanisa zima kwa wakati wote wa historia
yake tangu nyakati za mitume hadi
siku za mwisho kabla ya YESU kurudi mara ya pili .
II.
JE MALAIKA SABA HUWAKILISHA NINI? - Ni
“wajumbe au“uongozi wa kibinadamu wa kanisa katika kila kipindi Mungu
huzungumza na watu wake kupitia watumishi wake aliowateua
III.
JE KANISA LA KWANZA NI LIPI-KANISA LA KWANZA NI
LA EFESO.
UFUNUO 2:1, 7 Kwa
malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye
hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile
vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako,
na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao
mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa
ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba
umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu,
ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami
nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Lakini unalo neno hili,
kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. Yeye aliye
na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye,
nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu
IV.
JE KANISA LA EFESO LINAMAANISAHA NINI? –Linamaana
ya tamaniao au kupendeza
V.
JE KILIKUWA NI KIPINDI CHA KINANANI?-
Kilikuwa kipindi cha mitume (kanisa) walipeleka habali njema
ya wokovu Kwa ulimwengu wote,
VI.
JE KIPINDI CHA KANISA HILI KILIANZA WAKATI GANI?
Muda wa kanisa la EFESO ni kuanzia 31 A.D-100 AD
KANISA
LA PILI SMIRNA
UFUNUO 2:8-11 Na kwa
malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza
na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. Naijua dhiki yako na umaskini
wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi,
nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. Usiogope mambo yatakayokupata; tazama,
huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na
dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.Yeye
aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye
ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
i.
JE KANISA AU NENO SMIRNA HUMAANISHA NINI?-Neno
Smirna linamaanisha kitu kilichoinuka vizuri.Hiki ni kipindi cha pili cha
kanisa kilikuwa kimojawapo cha mateso na maumivu
ii.
JE KIPINDI CHA KANISA LA SMIRNA KILIANZA WAKATI
GANI?-Muda wakanisa la Smirna kilianza karibu na 100AD-313AD
iii.
JE SINAGOGI LA SHETANI WALIKUWA WAKINANI?-Sinagogi
la Shetani –Huenda walikuwani Wayahudi wa siku zile ambao mara kwa mara
waliwatesa wafuasi wa awali wa YESU.WARUMI 2:28-29
iv.
JE SIKU KUMI ZA MATESO ZILICHUKUA MUDA GANI?- Siku
kumi za za mateso Ni kipindi katika muda wa unabii.siku moja husimama Kwa mwaka
HESABU 14:34, EZEKIELI 4:6 kwa hiyo siku kumi za mateso ni miaka kumi ya MATESO
YA KISHENZI makali na ya mwisho yalikuwa chini ya mfalme DIOCLETIAN kati ya
mwaka 303 A.D -313 A.D
KANISA LA TATU PERGAMO
UFUNUO 2:12-17 Na kwa malaika wa kanisa lililoko
Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali
kuwili. Napajua
ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu,
wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu
wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. Lakini ninayo maneno machache
juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye
aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu
vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Vivyo hivyo wewe nawe unao watu
wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. Basi tubu; na usipotubu, naja kwako
upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. Yeye aliye na sikio,
na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa
baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo
limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
a.
JE KANISA AU NENO PERGAMO HUMAANISHA NINI? –humaanisha
mwinuko, kimo, urefu
b.
JE KIPINDI HIKI CHA KANISA KILIANZA LINI?-Kipindi
cha kanisa la Pergamo kuianza mwaka kati ya 313 A.D-538 A.D. huu ulikuwa wakati
ambao mateso yalikoma kabisa na hata mfalme Konstantino mwenyewe alijifanya kuwa Mkristo.
c.
JE ANTIPA NI WAKINANI?-Kanisa lilitukuzwa na kusifiwa
liliingia katika wakati wa hatari kubwa .Historia
haitufahamishi Mtu yoyote aliyeitwa antipa
lakini inaeleweka kuwa jina hili ni mfano wa kikundi cha watu katika kanisa
waliopoteza maisha yao Kwa sababu ya kuitetea kweli ya Mungu dhidi ya kiburi
cha Mapapa wa Rumi
ANTI -Maana
yake ni kupinga PA -inamaana ya baba au Papa
(pope) hivyo ANTIPA walikuwa ni wale
waliopinga kukua kwa uwezo na madai ya upapa (papacy) .
KANISA
LA NNE THIATIRA
(NI MWENDELEZO WA MAKANISA SABA)
UFUNUO
2:18-20
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya
ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na
miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. Nayajua matendo yako na upendo na
imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi
yale ya kwanza.Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli,
yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini
na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
JE JINA
THIATIRA LINAMAANISHA NINI?-Thiatira inamaana
ya kafara na toba
JE
KIPINDI HIKI KILIANZA WAKATI GANI?-Kilikuwa nikipindi cha Zama za Giza kilianza
MWAKA 538 A .D-1517 A.D (maelezo zaidi soma somo linalosema ZAMA ZA GIZA)
KANISA
LA TANO SARDI
UFUNUO
3:1-2 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi
andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota
saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe
mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa
yametimilika mbele za Mungu wangu.
JE JINA
SARDI LINAMAANISHA NINI–linamaanisha kanisa la Waprotestanti Wanamatengenezo?
JE
KANISA HILI LA SARDI LILIANZA WAKATI GANI?- Tunaweza
kuelewa kipindi hiki kuwa ni kuanzia
yapata mwaka 1517-1798 A.D Wakati MARTINI LURTHER HADI KUFIKIA 1798
JE NI
WATU GANI WASIOYATIA UCHAFU MAVAZI YAO?- Watu Wasioyatia mavazi yao uchafu
wanaweza kutajwa wacha Mungu waadilifu Kama LUTHER, COUNT NZINZENDORF, WESLEY,
WHITEFIELD NA WENGINE.
KANISA
LA SITA FILADELFIA
UFUNUO
3:7-8-13 Na kwa malaika wa kanisa
lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa
kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye,
naye afunga wala hapana afunguaye. Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa
mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo
nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. Tazama, nakupa walio wa sinagogi la
Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama,
nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. Kwa kuwa umelishika neno la subira
yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari
kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana
ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa
nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami
nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo
Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu
mwenyewe, lile jipya. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho
ayaambia makanisa
JE NENO
FILADELFIA HUMAANISHA ninI? -FILADELFIA humaanisha
upendo wa kindugu/ndugu,Hii ndio roho iliyolienea kanisa mwanzoni mwa nyakati
za mwisho.
JE
KANISA HILI LILIANZA WAKATI GANI? -Kipindi hiki kilianzia mnamo 1798 A.D- 1844
A.D.popote katika ulimwengu wakristo kanisa lilifurahishwa na maandiko na
mwamko waajabu, vyama vya BIBLIA vilianzishwa na maandiko na maandiko yalizidi
kuongezeka.
Kwa
mara ya kwanza watu walianza Kwa dhati kujifunza vitabu vya DANIELI NA UFUNUO
KANISA
LA SABA LAODIKIA
UFUNUO
3:14-22 Na kwa malaika wa kanisa
lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye
mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Nayajua
matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa
baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu,
wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri,
nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na
mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu
dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa,
aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate
kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua
mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.Yeye
ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi
nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio, na
alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
JE NENO
LAODIKIA LINAMAANISHA NINI? Laodikia maana yake ni kuwahukumu watu.
KANISA
hili linaishi duniani wakati wa kuhubiliwa kwa ujumbe wa malaika wa kwanza
UFUNGUO 14:7
Tangu
Yesu alipoanza kazi hii ya hukumu au kutakaswa kwa PATAKATIFU mwaka 1844 alipoingia
sehemu ya pili na ya mwisho ya yake danieli 8:14 tunaelewa kuwa kanisa la
laodikia litachukua kipindi cha kuanzia 1844 mpaka MWISHO WA HISTORIA YA
MWANADAMU WAKATI YESU AKAPORUDI MARA YA PILI.
MPENDWA SOMO LINALOFUATA NI
UNABII WA MUHURI SABA USIKOSE..
Amina don't pass without comment and share U will be blessed
ReplyDeleteubarikiwe
ReplyDelete