Monday, December 26, 2016

NYAKATI MBILI KUANZA PAMOJA;S/N 16


 

I.      VIPINDI VIWILI VYA KIUNABII KUANZA PAMOJA

UNABII WA MAJUMA 70

UNABII WA 2300


II.   KUMBUKA SIKU MOJA KIUNABII HUWAKILISHA MWAKA MMOJA

EZEKIELI 4:6. Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia

III.                        MUDA WA MAJUMA SABINI NA 2300
Muda wa Majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu ili kukomesha makosa ,na kushiliza dhambi ,na kufanya upatanisho kwa ajiri ya uovu , na kuleta haki ya milele ,na kutia Muhuri Maono na Unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu . DANIEL 9:24-27, Akawambia hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu ndipo patakatifu patakakapotakaswa. DANIELI 8:14

IV.                        UFAFANUZI WA MAJUMA SABINI

Majuma sabini yalianza Tangu agizo la utengenezaji na ujenzi upya wa Yerusalemu yaani mwaka (457KK soma Danieli 9:25, Ezira 7:11-16:) hadi Masihi mkuu (aya ya 25) ilikuwa ni miaka 483 au majuma 69(yaani majuma 7 jumlisha na majuma 62 soma aya 25) hii huleta hadi mwaka 27BK.(Kumbuka kutohesabu mwaka o) wakati Yesu alipoanza huduma yake duniani .hivyo hadi hapa yametumika majuma 69 kati ya yale majuma 70.tumesaliwa na juma moja tu ili kukamilisha yawe majuma 70 kamili ikimaanisha miaka saba
Hivyo hapa tunapata unabii wa aina mbili uliowekwa pamoja ukiwa mrefu kuliko mwingine .na mfupi ukiwa umekatwa kutoka kwa ulio mrefu .tukianza na agizo la kuujenga upya Yerusalemu mnamo mwaka 457 kk , miaka 2300 hutufikisha hadi mwaka 1844


V.   JUMA LA MWISHO LENYE SIKU SABA SAWA NA MIAKA SABA MAMBO MATATU YALIFANYIKA


27 BK Yesu alibatizwa na kuanza kuhubili na kufundisha


31 Bk Masihi akatiliwa mbali baada ya miaka mitatu ya huduma yake Danieli 9:26-27Marko 15:33


34BK Kifo cha stephano matendo 7:59-60 ndicho kilihitimisha unabii wa majuma sabini yaliyokuwa yametengwa kwa taifa la Israeli

VI.                        UNABII HUU wa 2300 Uliendelea baada ya kuisha ule wa majuma 70 ,kuna unabii wa makanisa saba ,mihuri saba na baragumu saba ulifuata ambao uliendelea hadi mwaka 1844.
1844 BK Ni mwisho wa siku 2300 za unabii na ni mwanzo wa hukumu ya upelelezi

MAELEZO YA ZIADA
KITABU CHA PAMBANO KUU SURA YA 18 UK 25

KICHWA CHA SOMO KINASEMA (INJIRI KWA ULIMWENGU)
Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa juma moja-miaka saba ya mwisho wa wakati wa wakati huo ulitilewa kwa ajiri ya wayahudi .Wakati huo wote tangu 27 AD mpaka 34
AD KRISTO na wanafunzi wake walieneza injiri kwa Wayahudi tu .agizo la kristo lilikuwa “Msiende kwenye njia ya mataifa wala katika miji ya samaria .lakini enendeni kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli MATHAYO 10:5-8
Na Kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka ya dhabihu kuu iliyotolewa huko kalwari dhabihu za wanyama zilikoma .huduma zote zilikuwa kivuli zilikwisha.
Miaka 490 ilitolewa kwa ajiri ya Wayahudi ilimalizika katika A.D 34 wakati huo kitendo cha Bunge kuu la kiyahudi cha kuamua kumwua
STEFANO kilifunga na kutia muhuli kanusho lao kwamba hawana haja na injiri tena, nao wakaanza kuwatesa wafuasi wa kristo na kuwaua.
Hapo sasa injiri ya wokovu ikapelekwa Kwa watu wa Mataifa katika ulimwengu wote, wanafunzi walilazimika kukimbia mateso kutoka Yerusalemu wakaenda huku na huko kila mahali wakilihubili lile neno MATENDO 8:4
Kumbuka tunaposema KK inawakilisha kabla ya kuzaliwa kwa YESU na BK baada ya kuzaliwa kwa YESU.usikose somo linalofuata linasema ZAMA ZA GIZA

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment