Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye
juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa
na vichwa vinne; akapewa mamlaka DANIELI 7:6 , Na baada ya zamani zako utainuka
ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa TATU WA SHABA,
utakaoitawala dunia yote DANIELI 2:39
1.
MNYAMA -Huwakilisha ufalme DANIELI 7:17
2.
MABAWA MANNE- Yaliwakilisha Mwendo wa haraka wa kushida kwake
3.
VICHWA VINNE -Huwakilisha mgawanyiko wa ufalme
katika falme nne mbalimbali baada ya kufa kwake
4.
CHUI NA MADINI YA SHABA –Huwakilisha utawala wa
WAYUNANI
5
UTAWALA huu ulianza kutawala Ulimwengu
tangu mwaka 331 B.C-168 B.C
6.
MFALME aliyetawala utawala huu alikuwa ni ALEKSANDA MKUU na baada ya kufa kwake
makamanda wake walitawala badala ya yake
7.
IFUATAYO NI HISTORIA FUPI
Ufalme
huu ndio wa mapaja ya shaba ya
sanamu uliokuwa ufalme wa Wayunani
uliosimamishwa kwa kushiinda upesi kwa ALEKSANDA MKUU .Chui ni mnyama
mdogo akilinganishwa na Dubu .tunasoma
…kama watu 47000 tu walikuwa katika jeshi la ALeksanda lilishinda jeshi kubwa sana lenye watu karibu milioni moja ,MABAWA manne yanaonyesha
mwendo wa haraka kushida ule wa babeli juu ya
sehemu ya jeshi liloshinda
.Aleksdanda alikuwa maarufu kwa
matengenezo yake ya hakili na mwendo wa haraka vichwa
vinne huonyesha mgawanyiko
wa ufalme wake katika
falme nne mbmbali
baada ya kufa kwake .
8.
Mpendwa usikose somo linalofuata maana
linazungumzia manyama wa nne ni mnyama wa kutisha sana maana hakufanana na mnyama yoyote Mungu
akubariki sana unapoendelea kuuchunguza ukweli huu wa biblia.
No comments:
Post a Comment