Monday, December 26, 2016

KIFUNGO KIREFU KULIKO VYOTE DUNIANI;S/N 19



a.     JE KIFUNGO HIKI KITACHUA MIAKA MINGAPI-JIBU ELFU MOJA

UFUNUO 20:1-31 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.

b.    JE NI KARAMU YA AINA GANI ITAFANYIKA KWA WAOVU BAADA TU YA WATAKATIFU KWENDA MBINGUNI

UFUNUO 19:17-18 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa

c.     JE MFUNGWA KATIKA KIFUNGO HIKI ATAKUWA NI NANI–JIBU NI SHETANI NA MALAIKA ZAKE

UFUNUO 20:2 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake

d.   JE GEREZA LA SHETANI LITAKUWA WAPI HAPA DUNIANI Jibu ni dunia yote itakuwa Gereza Lake

 

e.     JE BAADA YA KIFUNGO KUISHA NINI KITATOKEA?- SHETANI ATAFUNGULIWA KWA MUDA KIDOGO TU

UFUNUO 20:7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake

f.       JE SHETANI NA MALAIKA ZAKE WATACHA KAZI YA UDANGANYIFU ?-JIBU HATAACHA

 UFUNUO 20:8 Naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari

g.     JE SHETANI SHAMBULIO LAKE LA MWISHO NI LIPI ? –JIBU NI ZIDI YA NGOME YA MUNGU

UFUNUO 20:8-9 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala

h.    JE MWISHO WA SHETANI, MALAIKA ZAKE NA WATU ALIOWADANGANYA UTAKUWAJE?–JIBU WATACHOMWA MOTO NA KUWA MAJIVU KABISA NA HAWATAKUMBUKWA 

UFUNUO 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

i.       ANGALIA NUKUU HII KUTOKA KITABU CHA TUMAINI KUU KILICHAANDIKWA NA ELLEN G WHITE UK 402

KICHWA CHA HABARI ;MWISHO  MBAYA  WA WAOVU

Tabia ya Shetani haijabadilika .kwa mara nyingine , uasi kama mkondo  wa maji yenye nguvu  unaibuka .ataazimu kutoacha jitihada zake za mwisho  dhidi ya mfalme wa mbinguni ......EZEKIELI 28:6-8,16-19 nami nitakuangamiza  ewe kerubi ufunikaye  utoke katika mawe hayo ya moto ...nimekutupa chini ,nimekulaza mbele ya wafalme  wapate kukutazama ... nami nimekufanya kuwa majivu  juu ya nchi,machoni pa watu wote  wakutazamao...umekuwa kitu cha kutisha  wala hautakuwepo tena hata milele

Maana Bwana  ana ghadhabu  juu ya mataifa  yote  awanyeshee wasio haki  mitego ,moto na kiberiti na upepo wahari  na  viwe fungu  la kikombe chao  ISAYA 34:2 ZABURI 11:6.moto utashuka   mbinguni kwa Mungu .dunia itavunjika .miali ya moto  ulao unateketeza  utaibuka  kutoka kwenye miamba  yenywe itashika moto  vitu  vitaunguzwa kwa moto mkali ,Dunia pia  na matendo yaliyomo humo yataunguzwa 2 petro 3:10.uso  wa Dunia   unaonekana  kama  tope  kubwa  ziwa  kubwa  la moto  ni siku ya kisasi cha bwana ,mwaka  wa malipo ili kushindania sayuni ISAYA 34:8

Waovu wanaadhibiwa sawasawa na matendo yao .Shetani atateseka sio tu kwa uasi wake  lakini  kwa  dhambi zote alizosababisha  watu wa mungu  kutenda .hatimaye katika moto  waovu  wataangamizwa,mizizi na tawi –shetani  ndiye mzizi na wafuasi wake ni matawi .adhabu kamili  kwa uasi  wa sheria  imekwisha kutolewa ;hitaji  la haki  yamekwisha kutimizwa ,kazi  ya shetani  ya uharibifu imekomeshwa milele sasa viumbe wa Mumgu wamekombolewa milele kutoka kwenye majaribu yake

MPENDWA OMBA SANA ILI UOKOLEWE.USIKOSE SOMO LINALOFUATA MAISHA YA WATAKATI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 1000

 

:

 

No comments:

Post a Comment