Monday, December 26, 2016

YERUSALEMU MPYA UKISHUKA KUTOKA MBINGUNI;S/N 21



UFUNUO 21:1-2 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe

      I.            Angalia jinsi mji mtakatifu Yerusalemu ulivyo jengwa na unavyoonekana.

UFUNUO 21:10- 21   10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu; wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu. Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.  Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.  Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika. Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.  Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto. Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

II.            kuna masharti  mawili  ya huu  mji mtakatifu   

Moja hauhitaji jua wala mwezi ili kuuangaza mbili milango yake haitafungwa kamwe UFUNUO 21:23,25    Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. . Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.    

III.            Historia fupi baada ya miaka 1000 kumalizika.

Mwisho wa miaka 1000 kristo  atarudi  Duniani  akisindikizwa na waliokombolewa na jeshi la malaika ,Atawaamuru waovu waliokufa   kufufuka  ili wapokee hukumu yao.Watafufuka  watakuwa hawahesabiki  kama mchanga wa bahari ,wakiwa na dalili za ugonjwa na mauti .tofauti ilioje  baina ya wale waliofufuliwa  kwenye ufufuo wa kwanza

Kila  jicho  litakuwa  limegeuka  kuutazama utukufu wa Mwana  wa Mungu  kwa sauti  moja jeshi la waovu litasema : amebarikiwa  yeye ajaye  kwa jina la Bwana  MATHAYO 23:39 si upendo  utakaosababisha  tamko hili ,nguvu ya ukweli  italazimisha maneno  kutoka kwenye midomo   isiyoradhi kutamka kama ilivyokuwa  wakati walipolala katika  makaburi yao ,waovu watafufuliwa wakiwa na uadui ule ule  kwa  Kristo wakiwa  na roho ile ile ya uasi .hawatapata kipindi kingine  cha rehema  ili kurekebisha maisha yao yaliyopita

Nabii anasema “Miguu yake   itasimama juu ya mlima  wa MIZEITUNI nao mlima wa mizeituni utapasuka  katikati yake  ZEKARIA 14:4 Yerusalemu Mpya  utakaposhuka kutoka mbinguni , utakaa juu ya mahali palipotayarishwana Kristo na waytu wake  na malaika  wataingia kwenye Mji Mtakatifu 

Akiwa amekatiliwa mbali  na kazi  za udanganyifu ,mkuu wa uovu  atakuwa  na huzuni  na kuvunjika matumaini ,lakini waovu waliokufa  watakapofufuliwa  na atakapouona mkutano  mkubwa  ukiwa upande wake ,Matumaini  yake yatakuwa hai .hakusudii kushindwa  katika pambano kuu .atawapanga waliopotea chini ya bendela yake. kwa kumkataa Kristo  waliukubali utawala wa mwasi ,walikuwa tayari kutimiza amri zake.akiwa bado na hila zake  za awali . atakataa kukiri kuwa yeye ni shetani ,atadai kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa Dunia ambaye urithi wake ulinyanganywa pasipo  uhalali.atajionyesha mwenyewe kuwa ni mkombozi , akiwahakikishia wale aliowadanganya  kuwa ni uwezo wake uliowafufua  kutoka  kutoka makaburini mwao ,shetani  atawafanya waliodhaifu  kuwa na nguvu  na atawavuvia wote  kwa  uwezo wake kuwaongoza  kuutwaa mji wa Mungu ,

IV.            Shambulizi la mwisho dhidi ya Mungu                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                           

Shetani  atashauriana  na watu  hawa wenye  nguvu.watasema kwamba jeshi lililo  ndani ya mji  ni dogo  likilinganishwa na  la kwao na kwamba wataweza kushinda.mafundi wenye ujuzi  watatengeneza zana za vita .viongozi wa kijeshi  watapanga watu  mapenda vita  katika makundi na vikosi

Hatimaye amri ya kusonga mbele  itatolewa  na jeshi  lisilohesabika litasonga mbele ,jeshi hili litakuwa  kubwa kiasi kwamba  muungano  wa majeshi  ya zama zote  hautalingana nalo.shetani ataongoza kikosi cha mstari wa mbele ,wafalme wa mashujaa wake  watakuwa kwenye  msururu wake .kwa umakini wa kijeshi wanajeshi  wakiwa wamejipanga  kwenye mstari kulingana na vyeo vyao .watasonga mbele juu ya uso wa nchi uliobomolewa,,wakiuelekea mji wa Mungu .kwa amri ya  YESu malango ya  Yerusalemu Mpya  yatafungwa na majeshi ya Shetani  yatajipanga tayari  kwa mapambano

  V.            Hukumu yatolewa  dhidi ya  waasi (hapa kila mmoja ataonyeshwa  maisha yake na jinsi alivyomkataa kiristo)

kutawazwa kwa Kiristo kutafanyika  mbele ya mkutano wa wakazi  wa dunia na  wa mbinguni .na sasa  akiwa amevikwa  enzi na nguvu  mfamle wa wafalme atatoa  hukumu kwa waasi ambao waliasi sheria na  mfalme wa wafalme atatoa  hukumu kwa  waasi  ambao waliasi sheria  na  kuwatesa watu wake ufunuo 20:11-12……

Macho ya Yesu  yatakapowaangalia waovu ,wataitambua kila dhambi  ambayo waliwahi kuitenda .wataona ni wapi miguu yao ilitanga pembeni  mbali nanjia takatifui  .majaribu yenye kushawishi ambayo waliyawezesha kwa  kuendekeza dhambi,wajumbe  wa Mungu  waliopuuzwa,maonyo yaliyokataliwa ,mawimbi ya rehema  yaliyorudishwa nyuma  kwa ukaidi,moyo usiotubu yote yataonekana  kana kwamba  yaliandikwa kwa herufi za moto .Juu ya KITI CHA ENZI MSALABA UTAINULIWA. kama kulivyo kuonekana kwa SINEMA,yataonekena  mazingira  ya anguko  la ADAMU  na hatua zilizofuata  za mpango wa ukombozi;(KWA UFAFANUSI ZAIDI SOMA KITABU KILICHOANDIKWA NA ELLEN G WHITE CHA TUMAINI KUU ,SURA YA 42)

Baada ya kila mmoja muovu kujiona jinsi mbingu zilivyoshulikia wokovu wake ili aokolewe lakini akakataa yeye mwenye kila mmoja atakili akisema MUNGU HUKUMU ZAKO NI ZA KWELI NA ZA HAKI  na baada tu ya  tukio la kukili linalofuata ni waovu kuchomwa moto pamoja na SHETANI UFUNUO 20:10 ;

SOMO LINALOFUATA NI UNABII UNAOHUSU MAKANISA SABA.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment