Na ufalme wa nne utakuwa na
nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama
chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta. DANIELI 2:40 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama
wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno
ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga
mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza,
naye alikuwa na pembe kumi DANIELI
7:7
I.
SABABU ZINAZOFANYA MNYAMA HUYU WA NNE KUTISHA
SANA NA KUTOFANANA NA WANYAMA WENGINE WALIOTANGULIA NI HIZI
Alikuwa mwenye nguvu/Alikuwa na uwezo mwingi/ Alikuwa na
meno ya chuma makubwa sana alikula na kuvunja vunja vipande vipande/Alikuwa na
pembe kumi/Ulikuwa utawala wenye Utajiri /katili na kila aina ya maonevu
II.
MNYAMA HUWALIKISHA –Falme au Ufalme DANIELI 7:17
III.
HABARI NJEMA NYINGINE TUNAYOIPATA HAPA - Katika
utawala huu YESU ALIZALIWA
katika utawala huu WA RUMI YA UPAGANI
IV.
MNYAMA WA NNE WA KUTISHA NA MADINI YA CHUMA-
Huwakilisha utawala wa RUMI YA UPAGANI hii ilikuwa ENZI KUU YA NNE ULIMWENGUNI
V.
PEMBE KUMI ALIZOKUWA NAZO MNYAMA HUYU WA KUTISHA
-Zinawakilisha mgawanyiko wa DOLA YA RUMI YA
UPAGANI
katika majimbo kumi ambazo ni falme kumi
VI.
DOLA HII YA RUMI YA KIPAGANI ILIANZA KUTAWA ULIMWENGU -Tangu mwaka 168 B.C hadi 476A.D
VII.
IFUATAYO NI HISTORIA FUPI
RUMI YA KIPAGANI ilikuwa
ufalme wenye nguvu ulimwenguni
kuliko falme zingine zote
zilizotangulia .vilevile Rumi
ilitawala sehemu kubwa ya uso wa dunia kuliko falme zo zote zilizotangulia
ikaunganisha sehemu za AFRIKA,ASIA,ASIA NDOGO NA ULAYA
Ufalme
wa nne ambao kwao hakuna mnyama
aliyeumbwa kwa kutisha anayetosha kufananishwa nao Rumi ilifananishwa katika
sura ya pili na Miguu ya chuma.Pembe kumi ambazo ziliondoka katika
maanguko ya ufalme wa Warumi ……...kuonea watu bure kulikuwa kamili katika siku za Warumi …..kamwe
hapakuwapo ulimwenguni ufalme usio na
huruma wenye mamlaka hivi .Ulikizaja
kikombe chake cha udhalimu kwa kushiriki katika kusulubiwa kwa mwana wa MUNGU na kuwaua wakristo wa kwanza
VIII.
NAKUOMBA mpendwa usikose somo linalofuuta linalosema pembe
kumi na
pembe moja iliyokua zaidi ikawa na nguvu kuliko zingine pia kumbuka katika
utawala huu wa nne YESU KRISTO alizaliwa na baadaye alipomaliza kazi yake
alirudi mbinguni mada hii ya kuzaliwa kwa Yesu tutajifunza sana
tutakapofika danieli sura ya 9.Mungu akubariki sana:
No comments:
Post a Comment