Monday, December 19, 2016

JE UNAJUA KUNA WANYAMA WANNE WENYE MAAJABU NA MADINI MANNE YANAYOFANANA NAO ?-S/N 10



Mpendwa katika Bwana tunaenda kujifunza UNABII wa DANIELI sura ya PILI na sura ya SABA nakuomba ufuatilie MNYAMA mmoja hadi mwingine.

      I.            LENGO LA KUJIFUNZA  SURA YA PILI NA YA SABA NI HILI

SANAMU YA  SURA  YA  PILI - Inaeleza historia ya dunia  kwa  namna ihusuyo tu serikali  za nchi ;MAONO YA SURA  YA SABA  ni  mfano wa falme nne za dunia katika  mambo ya maana  ya kiroho kama yalivyoelezwa  kwa kazi ya MUNGU na watu wake;

MNYAMA WA KWANZA NI SIMBA- Alifananishwa na madini ya dhahabu (Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.Wa kwanza alikuwa kama SIMBA, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu. DANIELI 7:2-4 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme. Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;  na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu DANIELI 2:36-38)

   II.            MNYAMA ANAWAKILISHA NINI? DANIELI 7:17

Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.

JIBU MNYAMA ANAWAKILISHA- Falme mbalimbali zitakazotokea Duniani

III.            KWA NINI WANYAMA HAWA WALITOKEA BAHARI AU MAJINI?

JE MAJI YANAWAKILISHA NINI UFUNUO 17:15

Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.

JIBU MAJI HUWAKILISHA -Jamaa na Makutano na Mataifa na Lugha

IV.            SIMBA NA DHAHABU iliwakilisha Enzi kuu ya kwanza kutawala Ulimwengu au Dunia

   V.            MABAWA YA TAI aliyokuwa nayo simba huonyesha wepesi wa ushindi wa Babeli

VI.            MADINI YA DHAHABU yaliwakilisha utajiri ,uwezo na utukufu mwingi uliokuwa Babeli

VII.            UTAWALA huu ulinza mnamo mwaka wa 605  B.C—538 B.C

VIII.            Wafalme waliotawala ENZI KUU YA KWANZA aliitwa NEBUKADREZA      alitawala miaka arobaini na mitatu.alirithiwa na wafalme watano wadhaifu  sana ambao wa  mwisho ndiye BELISHAZA (tazama sura ya 5)

IX.            IFUATAYO NI HISTORI FUPI YA

Enzi kuu ya kwanza kutawala ulimwengu

UFALME wa Babeli ulianzishwa na  NIMRODI kwa kumwasi Mungu (Mwanzo 10:8-10) ulizidi kukua katika siku za NEBUKADREZA,ukawa  ufalme  wenye  utajiri na utukufu mwingi katika ulimwengu.Nebukadreza mjenzi  mstadi aliupamba mji huu  mkuu kwa matengenezo  yasiyo yakawaida  baadaye twamsikia akisema mji huu sio babeli mkuu  nilioujenga mimi?( Danieli 4:30) ulikuwa mji  wa ajabu katika ulimwengu wa kale pia ufalme wa kwanza  simba  huleta jawabu katika  kichwa  cha dhahabu cha sanamu  ya sura ya pili  ambao ulikuwa ufalme wa babeli yeremia  alibashiria Yuda kuja kwa jeshi la Babeli kushambulia  akiwafananisha na kuja kwa simba mwenye  kuangamiza Yeremia 4:7, 21:7 mabawa huonyesha wepesi wa jeshi wa babeli Habakuki 1:6-8 alisema ya kwamba farasi  wa wakaldayo ni wepesi kuliko chui………… huruka  kama tai afanyae haraka ale

Lengo lingine la kujifunza unabii huu utatusaidia kujua hiStoria yetu kwamba tumetoka wapi na tunaenda wapi ili tujue tuchukue tahadhali dhidi ya mafundisho ya uongo

   X.            Pia kupitia historia hii ya falme mbalimbali tutajifunza historia ya Makanisa mbalimbali kwamba yametoka wapi kwa nini leo ni mengi sana na kila kanisa hudai liko sahihi je ni kweli?

XI.            Mpendwa fuatilia kwa makini utajua tu usikose hata somo moja  Mungu akubariki SOMO LA PILI LITAHUSU MNYAMA DUBU USIKOSE

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment