Monday, December 26, 2016

UNABII WA MAKANISA SABA ;S/N 22

UFUATAO NI MCHANGANUO WA KANISA  MOJA  HADI JINGINE.

UFUNUO 1:3-4,20 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

KANISA LA KWANZA LA EFESO;

      I.            JE MAKANISA SABA YANAMAANISHA NINI?

MAANA YA KWANZA YA MAKANISA SABA- Majina ya makanisa Saba ni mfano wa kanisa katika zama mbalimbali za kikristo

MAANA YA PILI YA MAKANISA SABA-Ni mifano iliyotumiwa huonyesha hali ya kanisa Kwa nyakati tofauti katika historia ya ulimwengu.

MAANA YA TATU YA MAKANISA SABA- Makanisa saba yanasimama badala ya kanisa  zima  kwa wakati wote  wa historia  yake tangu  nyakati za mitume  hadi  siku za mwisho kabla ya YESU kurudi mara ya pili .

   II.            JE MALAIKA SABA HUWAKILISHA NINI? - Ni “wajumbe au“uongozi wa kibinadamu wa kanisa katika kila kipindi Mungu huzungumza na watu wake kupitia watumishi wake aliowateua

III.            JE KANISA LA KWANZA NI LIPI-KANISA LA KWANZA NI LA EFESO.

UFUNUO 2:1, 7 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu

IV.            JE KANISA LA EFESO LINAMAANISAHA NINI? –Linamaana ya tamaniao au kupendeza

   V.            JE KILIKUWA NI KIPINDI CHA KINANANI?-

Kilikuwa kipindi cha mitume (kanisa) walipeleka habali njema ya wokovu Kwa ulimwengu wote,

VI.            JE KIPINDI CHA KANISA HILI KILIANZA WAKATI GANI?

Muda wa kanisa la EFESO ni kuanzia 31 A.D-100 AD


KANISA LA PILI SMIRNA

UFUNUO 2:8-11 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

             i.            JE KANISA AU NENO SMIRNA HUMAANISHA NINI?-Neno Smirna linamaanisha kitu kilichoinuka vizuri.Hiki ni kipindi cha pili cha kanisa kilikuwa kimojawapo cha mateso na maumivu

           ii.            JE KIPINDI CHA KANISA LA SMIRNA KILIANZA WAKATI GANI?-Muda wakanisa la Smirna kilianza karibu na 100AD-313AD

 

        iii.            JE SINAGOGI LA SHETANI WALIKUWA WAKINANI?-Sinagogi la Shetani –Huenda walikuwani Wayahudi wa siku zile ambao mara kwa mara waliwatesa wafuasi wa awali wa YESU.WARUMI 2:28-29

         iv.            JE SIKU KUMI ZA MATESO ZILICHUKUA MUDA GANI?- Siku kumi za za mateso Ni kipindi katika muda wa unabii.siku moja husimama Kwa mwaka HESABU 14:34, EZEKIELI 4:6 kwa hiyo siku kumi za mateso ni miaka kumi ya MATESO YA KISHENZI makali na ya mwisho yalikuwa chini ya mfalme DIOCLETIAN kati ya mwaka 303 A.D -313 A.D

 

KANISA LA TATU PERGAMO

UFUNUO 2:12-17 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.  Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.  Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.  Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.  Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

a.     JE KANISA AU NENO PERGAMO HUMAANISHA NINI? –humaanisha mwinuko, kimo, urefu

b.   JE KIPINDI HIKI CHA KANISA KILIANZA LINI?-Kipindi cha kanisa la Pergamo kuianza mwaka kati ya 313 A.D-538 A.D. huu ulikuwa wakati ambao mateso yalikoma kabisa na hata mfalme Konstantino mwenyewe alijifanya kuwa Mkristo.

c.     JE ANTIPA NI WAKINANI?-Kanisa lilitukuzwa na kusifiwa liliingia katika wakati wa hatari kubwa .Historia haitufahamishi Mtu yoyote aliyeitwa antipa lakini inaeleweka kuwa jina hili ni mfano wa kikundi cha watu katika kanisa waliopoteza maisha yao Kwa sababu ya kuitetea kweli ya Mungu dhidi ya kiburi cha Mapapa wa Rumi

ANTI -Maana yake ni kupinga PA -inamaana ya baba au Papa (pope) hivyo ANTIPA walikuwa ni wale waliopinga kukua kwa uwezo na madai ya upapa (papacy)  .


KANISA LA NNE THIATIRA

 (NI MWENDELEZO WA MAKANISA SABA)

UFUNUO 2:18-20 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.

JE JINA THIATIRA LINAMAANISHA NINI?-Thiatira inamaana ya kafara na toba

JE KIPINDI HIKI KILIANZA WAKATI GANI?-Kilikuwa nikipindi cha Zama za Giza kilianza MWAKA 538 A .D-1517 A.D (maelezo zaidi soma somo linalosema ZAMA ZA GIZA)

 

KANISA LA TANO SARDI

UFUNUO 3:1-2 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.  Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.

JE JINA SARDI LINAMAANISHA NINI–linamaanisha kanisa la Waprotestanti Wanamatengenezo?

JE KANISA HILI LA SARDI LILIANZA WAKATI GANI?- Tunaweza kuelewa kipindi hiki   kuwa ni kuanzia yapata mwaka 1517-1798 A.D Wakati MARTINI LURTHER HADI KUFIKIA 1798

JE NI WATU GANI WASIOYATIA UCHAFU MAVAZI YAO?- Watu Wasioyatia mavazi yao uchafu wanaweza kutajwa wacha Mungu waadilifu Kama LUTHER, COUNT NZINZENDORF, WESLEY, WHITEFIELD NA WENGINE.

 

KANISA LA SITA FILADELFIA

UFUNUO 3:7-8-13 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.  Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.  Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa

JE NENO FILADELFIA HUMAANISHA ninI? -FILADELFIA humaanisha upendo wa kindugu/ndugu,Hii ndio roho iliyolienea kanisa mwanzoni mwa nyakati za mwisho.

JE KANISA HILI LILIANZA WAKATI GANI? -Kipindi hiki kilianzia mnamo 1798 A.D- 1844 A.D.popote katika ulimwengu wakristo kanisa lilifurahishwa na maandiko na mwamko waajabu, vyama vya BIBLIA vilianzishwa na maandiko na maandiko yalizidi kuongezeka.

Kwa mara ya kwanza watu walianza Kwa dhati kujifunza vitabu vya DANIELI NA UFUNUO

KANISA LA SABA LAODIKIA

UFUNUO 3:14-22 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.  Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.  Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.  Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

JE NENO LAODIKIA LINAMAANISHA NINI? Laodikia maana yake ni kuwahukumu watu.

KANISA hili linaishi duniani wakati wa kuhubiliwa kwa ujumbe wa malaika wa kwanza UFUNGUO 14:7

Tangu Yesu alipoanza kazi hii ya hukumu au kutakaswa kwa PATAKATIFU mwaka 1844 alipoingia sehemu ya pili na ya mwisho ya yake danieli 8:14 tunaelewa kuwa kanisa la laodikia litachukua kipindi cha kuanzia 1844 mpaka MWISHO WA HISTORIA YA MWANADAMU WAKATI YESU AKAPORUDI MARA YA PILI.

MPENDWA SOMO LINALOFUATA  NI  UNABII  WA  MUHURI SABA USIKOSE..

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2 comments: