Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne
watakaotokea dunia..............na habari za zile pembe kumi zilizokuwa
kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka
pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo
kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake. Nikatazama, na pembe iyo hiyo
ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda , Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye
atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na
sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu
wakati
DANIELI 7 ;17-22,25 . Na kama vile
ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi,
na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake
zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na
udongo wa matope. Na kama vidole vya zile nyayo
vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una
nguvu, na nusu yake umevunjika DANIELI
2:;41-42
Jambo
la kuzingatia ni hili baada ya utawala huu wa RUMI YA UPAGANI ulifuata
RUMI
YA UKRISTO ina maana kwamba Rumi ya upangani iliungana na Rumi ya
ukristo kuwa kitu kimoja
1.
PEMBE KUMI
kwanza zilitokana na ufalme wa nne wa RUMI YA UPAGANI ufalme huu
haukutawaliwa na mwingine ila ilipofikia mwisho iligawanyika katika falme
kumi
2.
PEMBE KUMI NA VIDOLE KUMI - Zinawakilisha
ufalme wa RUMI YA UKRISTO
3.
FALME TATU -Zilizoangushwa kwa kushambuliwa na
pembe ndogo ambazo ni HERULI,VANDALS,NA OSTROGOTHS
4.
FALME SABA zilizobaki ambazo ni
England,France,Spain,Portugal,Germany,Switzeland ,Italy
5.
UTAWALA HUU
WA RUMI YA UKRISTO ulianza kutawala dunia tangu mwaka 476 A.D
utaende hadi mwisho wa kufunga
historia ya ulimwengu na baada tu ya
utawala huu YESU anakuja katika Mawingu
ya Mbinguni;
6.
PEMBE NDOGO NINANI? JIFUNZE YAFUATAYO
MAMBO SITA YANAYOHUSU PEMBE NDOGO
1. PEMBE NDOGO, ATATOKEA KATIKA
UFALME WA WARUMI, LAKINI ATAKUWA MBALI NAZO.
Hivyo Pembe ndogo si ufalme tu Kama falme zingine kumi
lakini ni NGUVU ZA KIDINI ZILIZOINUKA MIONGONI MWA SERIKARI Maneno ya askofu wa Rumi kwanza yalionekana
kama yatoka kwa mshauri na ndugu mkubwa Miaka
ilipoendelea mbele maneno yake yalianza kupokelewa kama yatoka kwa baba.Ufalme
wa Rumi
ulipozidi kudhoofika askofu (sasa aitwaye PAPA maana yake (baba
katika kilatini akaanza kuheshimiwa kama BWANA Mwisho
yalifanywa madai ya kiburi ya kuwa PAPA ni MUNGU hapa duniani.
2, ATAPIGANA KWA NGUVU KUTIISHA FALME TATU ZILIZOPINGA NIA
YAKE.
Falme tatu zilizongolewa kabisa mbele ya papa Ni HERULI
chini ya Odoace, VANDALi Na OSTROGOSTHS chini ya Theodoric
3. ATANENA MANENO MAKUU (YA KUFURU –TAZAMA UFUNUO 13:5) JUU
YAKE MUNGU ALIYE JUU
Pembe ndogo itanena maneno mkuu kinyume chake aliye juu
.madai yake ya kiburi na kufuru yaliyofanywa na PAPA yasemwayo hapa yametwaliwa
kutoka katika FERRIS ECCLESIASTICAL DICTIONARY
Papa ni mwenye kuheshimiwa
sana na aliyetukuzwa ,yeye si mtu
tu ,bali ni kama aliye Mungu ,na kasisi wa Mungu …..PAPA
huvishwa taji iliyo Na matabaka MATATU ya
kuwa Ni mfalme wa Mbinguni na wa Duniani na AHERA
4. ATAWADHOOFISHA.MAANA YAKE ATAWATESA WATAKATIFU ALIYE JUU
Wakati wa zama za giza ,ambao ulianza katika mwaka 538 B.K kanisa la kirumi na
madhehebu yake liliwatesa wakristo wapatao
50,000,000 mpaka kufa .habari
hii ya kuogofya ni historia
moja ya giza kabisa katika historia ya mwanadamu .
5. ATAJARIBU KUBADIILI MAJIRA NA SHERIA YA MUNGU.
Pembe ndogo
atajaribu kubadili nyakati
na na sheria ya Mungu tutumie maneno machache kutoka
katika ROMANI COTHOLIC PROMTA
BIBLOTHECA YALIYOANDIKWA NA FERRARIS;Papa Ni mwenye mamlaka makuu
na uweza hata aweza kugeuza?(kubadili) kueleza au kutafsiri sheria takatifu VOL
,UK,29 KATIKA KATEKISIMU ZA KANISA LA
KIRUMI
zitumiwazo kuwafundisha wanafunzi sheria ya Mungu imegeuzwa kidogo ,kwa sababu hiyo amri ya pili
inayokataza kuabudu sanamu
imefutwa .Amri ya nne imefupishwa
ili kuendeleza kushika SIKU YA KWANZA YA JUMA
(sunday)mahali pa sabato ya kweli.Amri ya kumi imegawanywa kuwa amri mbili.
6. ATAENDELEA KWA WAKATI NA NYAKATI MBILI NA NUSU YA WAKATI
AU MIAKA MITATU NA NUSU,
Siku moja katika unabii huwakilisha –mwaka mmoja (EZEKIELI
4:6, HESABU 14:24) katika UFUNUO 12:6, 12:14, 13:5
JASTINIA alitoa amri
katika mwaka wa 538 B.K akimpa papa mamlaka yasiyo na mpaka juu ya makanisa yote.amri hiyo ilitimilizwa katika mwaka wa 538 B.K wakati pembe tatu zilizopinga kanisa la Rumi na madhehebu yake zilipoangamizwa kwa vita.hivyo wakati wa
kuanza miaka 1260 baadaye ,PAPA
ALIPOTEZA MAMLAKA YAKE KWA MUDA KATIKA
FEBRUARI 20,1798 BERTHIER JEMEDARI WA
JESHI LA UFARANSA CHINI YA NAPOLEONI alimteka Papa na kumfunga katika Rumi,ndio ulikuwa mwisho
wa kanisa la Rumi na madhehebu yake kwa
muda .baada ya wakati huo hakukutokea
mateso ya watakatifu ULAYA
walikuwa huru kumwabudu MUNGU.,
MPENDWA TUTAENDELEA TENA BAADAYE SURA YA 9
INAYOHUSU UNABII WA MAJUMA SABINI NA UNABII WA SIKU 2300.MUNGU AKUBARIKI AMINA
No comments:
Post a Comment