i.
PASAKA NINI?
Pasaka
ilikuwa imeanzishwa kuwa ukumbusho wakukombolewa kwa waisraeli kutoka katika utumwa
wa Misri.
ii.
CHAZO AU CHIMBUKO LA PASAKA
|
kila
mtu atatwaa mwakondoo…tena mtamla hivi
mtakuwa mmefungwa viuno vyenu , mmevaa viatu vyenu miguuni ,na fimbo zenu mikononi mwenu
nanyi mtamla kwa haraka ni pasaka
kwa bwana KUTOKA 12:3
iii.
ZIFUATAZO NI HATUA TATU AMBAZO KILA MTU
ANAYEAZIMISHA PASAKA ANAPASWA KUZIFUATA;
HATUA
YA KWANZA NI KUTAWAZANA MIGUU ;YOHANA 13 :1-15
Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya
kuwa saa yake imefika,........... aliondoka chakulani;
akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. Kisha akatia
maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile
kitambaa alichojifunga........... Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu,
nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. sababu kubwa ya kutawaza miguu ni hii hapa
Katika
moyo wa mwanadamu kuna hali ya kujitukuza
mwenyewe na kujiona kuwa bora kuliko mwenzake;kujipendelea ,kutafuta
ukuu; na mara nyingi huwa na matokeo ya
dhana potovu na chuki.huduma ya kutawazana
inayotangulia meza ya bwana
inakusudiwa kumwondoa mtu katika ubinafsi,kumshusha kutoka katika
kujiinua nafsi,na kumleta katika unyenyekevu utakaomwezesha kumhudumia ndugu
yake mwonaji Mtakatifu kutoka mbinguni
huwapo katika huduma hii kuifanya
kuwa ya kutafakari mambo ya kiroho
kujutia dhambi.kristo huwapo kubadilisha mkondo wa mitiririko wa mawazo ya
ubinafsi
HATUA YA PILI
KUNYWA DIVAI ;LUKA 22:17,201
Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki,
mgawanye ninyi kwa ninyi; Kikombe nacho
vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu
yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
HATUA
YA TATU NI KULA MKATE LUKA 22:19
Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema,
[Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho
wangu.
iv.
NINI MAANA YA MEZA YA BWANA AU PASAKA AMBAYO YESU ALISHIRIKI?
Meza ya
Bwana ilianzishwa kuwa ukumbusho wa kukombolewa kulikoletwa kama matokeo ya
kifo cha kristo adhimisho la agizo hili ndiyo njia ya kutukumbusha daima kazi
yake kuu kwa ajiri ya wokovu wetu
SABABU
YA KUAZIMISHA MEZA YA BWANA
Lakini
huduma ya meza ya Bwana haikukusudiwa kuwa wakati wa huzuni .kadiri wanafunzi
wa Yesu watapokusanyika mezani pa Bwana hawapaswi kuomboleza kwa ajiri ya
upungufu wao. hawapaswi kutafakari tofauti zao
na wenzao huduma ya
kutawazana imeshugulikia yote hayo .sasa
wanakuja kukutana na kristo,hawapaswi
kusimama kwenye kivuli cha msalaba bali
katika mwanga wake wa wokovu,wanapaswa kufungua mioyo yao kwa nuru itokayo jua lakini wanapaswa kusikia maneno yake
v.
WANAORUHUSIWA KUSHIRIKI
katika pasaka ni watu wote waliobatizwa kwa maji mengi Watu ambao
hawaruhusiwi kushiriki pasaka ni wale walioondolewa kwenye vitabu vya ushirika au vya kanisa kutokana na kutenda dhambi ya kulidhalilisha kanisa hadi
hapo watakapobatizwa tena Watu wengine wasioruhusiwa ni watoto
na watu wazima ambao hawajabatizwa .
TAHADHALi
mpendwa kama hizo hatua tatu hushiriki wakati wa kuazimisha pasaka jua kabisa
pasaka unayoazimisha siyo sahihi chukua hatu pia pasaka ya Bwana siyo ya
kuchinja ngome ,kuku,mbuzi ,kushona nguo, na mengineyo
No comments:
Post a Comment