HABAKUKI 2:15 :Ole wake yeye
ampaye jirani yake kileo ,wewe utiaye
sumu yako,na kumlevya pia ,ili
kuutazama uchi wao
I.
UNYWAJI WA
POMBE KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORI YA MWANADAMU,MWANZO 9:20-21
Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa
divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake
Nuhu: Akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake
II.
ORODHA YA
MADHARA YANAYOTOKANA NA MATUMIZI YA POMBE MITHALI 23:29-35,
Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani
mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana
kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo
ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma
kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona
mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye
katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.Utasema, Wamenichapa
wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta
tena. Mithali 20:11 Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi;
Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima
III.
JE KUNA
MTU YOYOTE ANAYERUHUSIWA KUNYWA POMBE
WAEFESO 5:18,
Tena
msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho
Walawi 10:9 Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe,
wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba
msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;
IV.
JE
WATUMISHI WA MUNGU WANARUHUSIWA KUNYWA POMBE ISAYA 28:7
Lakini hawa nao wamekosa kwa divai, wamepotea kwa kileo;
kuhani na nabii wamekosa kwa kileo, wamemezwa kwa divai, wamepotea kwa kileo;
hukosa katika maono, hujikwaa katika hukum,Isaya 56:10-12Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni
mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi. Naam,
mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza
kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila
mmoja kwa faida yake, toka pande zote. Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe
sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi.
V.
JE MUNGU
ANATOA OLE GANI KWA WATUMIAJI WA POMBE
ISAYA 5:11 ,22
Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo;
wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao
Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu
kuchanganya vileo
VI.
JE MUNGU
ANASEMAJE JUU YA WATU WOTE WANAOTUMI POMBE WAGALATI 5:19-21
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati,
uchafu, ufisadi,ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina,
faraka, uzushi,husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo
nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo
ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu
Katika
kitabu kilichoandikwa na Ellen g white
KUTAYARISHA NJIA SEHEMU YA
KWANZA, SURA 16 NJIA KUU YA SHETANI KULETA UHARIBIFU, UK 117-121 ANASEMA
Shetani
aliwakusanya malaika wabaya pamoja kutafuta njia ya kufanya uovu mkubwa iwezekanavyo kwa wanadamu.mashauri yakatolewa
moja moja ,mpaka mwishowe shetani mwenyewe akafikiri njia .akapenda kuyatwaa
matunda ya mzabibu ,pia ngano na vitu vingine vilivyotolewa na Mungu chakula
na kuvigeuza kuwa sumu ambayo
ingeuharibu uwezo wa mwanadamu wa mwili ,akili ,na tabia ya moyoni na hivyo
atazishinda akili za kupambanua mema na mabaya hata shetani apate kutawala
kabisa.,,,,,,,,,,,kwa mvuto wa kinywaji
wanywacho watu huongozwa kutenda mambo
ambayo kama wasingelikuwa
wameonja kitu chenye kulevya na kurusha akili wangeepuka kwa hofu kuyatenda wakiwa katika
hali ya kulewa wako kwenye mamlaka ya
shetaninao husaidiana naye DIVAI ambayo
kristo aliifanyia kwa maji katika karamu ya arusi ya kana ilikuwa majimaji
matupu ya zabibu.
No comments:
Post a Comment