NAMNA
YA KUFUNGA
SOMO
HILI LINA VIPENGELE VITATU.
a.
Nini maana ya kufunga
b.
Aina za kufunga au saumu
c.
Mambo ya kuzingatia unapokuwa umefunga
A. NINI
MAANA YA KUFUNGA AU SAUMU
MAANA
YA KWANZA –Kufunga kunakoamriwa katika neno la Mungu si kufunga
kwa kawaida tu.Asili yake si
kukataa chakula ,kujivika nguo za magunia ,na kujitia majivu kichwani
.Yeye afungaye kwa kuwa
amehuzunishwa moyoni kwa ajiri ya dhambi zake ,Hataki kuonyesha
kwa wengine kufunga kwake .
MAANA
YA PILI-Kufunga kule kunakotakiwa kwetu na Mungu ,si kwa kuutesa
mwili kwa ajiri ya dhambi rohoni ;Ila
kutusaidia kufahamu hali yetu ya dhambi
jinsi ilivyo mbaya mno,Ili tujidhili mioyoni mwetu mbele za Mungu na kupokea
neema zake na masamaha yake
.Aliwaamuru Waisraeli hivi .Rarueni mioyo yenu wala si mavazi yenu
mkamrudie Bwana Mungu wenu YOELI 2:13
B.
KUNA AINA NNE ZA KUFUNGA AU SAUMU
i.
KUFUNGA SIKU 1
Ndipo wana Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea,
wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za Bwana, wakafunga siku hiyo
hata jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za
Bwana
waamuzi 20:26, Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji
na kuyamimina mbele za Bwana; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia
Bwana dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa 1
SAMWELI 7:6,
ii.
KUFUNGA SIKU 3
Uende
Ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu;
msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu
tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami
nikiangamia, na niangamie. ESTA 4:16
iii.
KUFUNGA SIKU 21
Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza
muda wa majuma matatu kamili. Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai
haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu
kamili yalipotimia DANIELI
10:2-3
iv.
KUFUNGA SIKU 40
Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na
Ibilisi.Akafunga siku arobaini mchana na
usiku, mwisho akaona njaa Mathayo
4:1-2, kutoka 9:9,18, Naye
alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala
hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo
amri kumi kutoka 34:28
C.
JE MAMBO GANI YAKUZINGATIA UNAPOFUNGA/SAUMU
ISAYA 58:5-10 Je!
Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha
nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu
chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana? Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii?
Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa,
na kwamba mvunje kila nira? e! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na
kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike
nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? dipo nuru yako
itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako
itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri
Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri
.HAYA NDIYO MAMBO MANNE YA KUZINGATIA.
1.
TAHADHALI Kutokula chakula kabisa hasa mfungo wa
muda mrefu haishauriwi kula kiasi kwa ajiri ya afya yako chakula cha
kawaida siyo cha anasa kama DANIELI ALIVYOFANYA KATIKA SIKU 21
2.
Kufungua vifungo vya uovu,au kuungama dhambi
zako zote
3.
Kuzilegeza kamba za nira
4. Kuwapa
chakula wahitaji katika hili tumia angalau sehemu ya bajeti yako uliyokuwa
unatumia kabla haujafunga kuwapa
wahitaji au masikini.
JE
KUNAFAIDA GANI TUNAZOZIPATA KUTOKANA NA MFUNGO
1.
Utamwita Bwana naye atakuitikia
2. Atakusamehe
dhambi zako
3. Utapata
afya njema
4.
Atakujibu maombi yote uombayo sawasawa na
mapenzi ya Mungu.
No comments:
Post a Comment