Monday, December 19, 2016

ULINZI ULIO IMARA DUNIANI:-SOMO NO;2


 
 
Mpendwa ulinzi huu ni wa peke yake:Bwana asipoilinda nyumba/ mji wako  walindao wanakesha bure.
JIFUNZE JINSI ULINZI WA MUNGU ULIVYO
                   i.            USIOGOPE
ISAYA 41:10-13, ISAYA 59:1
Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni      Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.
                 ii.            WALINZI WETU NI MALAIKA WA MUNGU
ZABURI 91:11-12,34:7, WAEBRANIA 1:14  Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe
              iii.            HUPASWI  KUHOFU SHAMBULIO LOLOTE LIWE LA GHAFULA  AU SIO
ZABURI 91:5-10 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,  Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe. Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki. Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako
               iv.            UKIMWAMINI MUNGU ULINZI WA MUNGU NI WA HAKIKA SOMA MIFANO HII
2 WAFALME 6:13-23- SOMA hili fungu lote utaona Elisha avyopambana na jeshi la watu wengi na kushinda kwa kishindo kikubwa
DANIELI 6:18-24 -SOMA utaona Danieli alivyoshinda japokuwa walimtupa kwenye tundu la simba ili auawe na simba 
TAHADHALI usiwategemee wanadamu /wala mazindiko ya uganga /uchawi aina yoyote . maana vitu kama hivyo kwa Mungu havifanyi kazi yoyote.YEREMIA 17:5-Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
 


No comments:

Post a Comment