JE MBINGUNI NI MAHALI HALISI-JIBU NDIO
YOHANA 14:1-3, Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na
mimi.Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana
naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja
tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. WAEBRANIA
11:16
Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya
mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea
mji.
VITU AU MAMBO YATAYOKUWA YANAENDELEA MINGUNI BAADA YA WAKATIFU
KUFIKA
i.
WAKATIFU WATAKAPOFIKA MBINGUNI WATAKARIBISHWA NA
YESU
Mathayo
25:34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko
mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme
mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu
ii.
YESU ATAWAVISHA TAJI YA USHINDI
Watapewa taji ya uzima “thawabu yaani, utukufu ule wa mbinguni,
watakaopewa washindi wale, italingana na kiwango walichoweza kuiwakilisha TABIA
YA KIRISTO katika Ulimwengu huu..Taji ya Uzima itangaa sana au itakuwa na mwanga uliofifia ,itametameta ikiwa na nyota nyingi,au itaangazwa kwa johari
chache sana ,kulingana na mwenendo wetu wenyewe(OHC 123) ,2 WAKORINTHO 9:6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba;
apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
iii.
WATAKATIFU WATAFANYIWA KARAMU KUBWA YENYE VINONO
ISAYA 25:66 Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa
yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake,
karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo
wake, iliyochujwa sana.
iv.
KAZI MOJAWAPO WATAKAZOKUWA WANAZIFANYA
WATAKATIFU NI KUPITIA HUKUMU AMBAZO YESU AMEKWISHA KUZITOLEA MAAMUZI,HUO NDIO
UTAKUWA WAKATI WAKUTAMBUANA KWA NINI FURANI HAKUOKOLEWA
1 WAKORINTHO 6:2-3 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na
ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo
ndogo? Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha
haya UFUNUO
20:4-6Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi
juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa
ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia
yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya
nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo
miaka elfu. , (1 WAKORINTHO 4:5)
v.
WATU WATAKUWA NA MAUMBILE GANI?
Urefu wa karibu futi kumi na mbili” wakiwa wemerejeshwa
kwenye mti wa uzima katika edeni ile
iliyopotea zamani sana wale
waliokombolewa wataendelea kukua (malaki
4:2) na kufikia kimo kamili cha jamii
ya wanadamu wa asili katika utukufu wake (gw 676) yeye adamu alikuwa na
erefu wa zaidi ya mara mbili kuliko
ule wa mwanadamu wanaoishi sasa
na mwili wake uliumbika ukiwa na uwiano
mzuri
vi.
JE MAUMIVU, KIFO YATAKUWAPO?
Maumivu hayawezi kuwako katika mazingira yale ya mbinguni
.hapatakuwepo na machozi tena ,wala misafara
ya mazishi ,wala tepe za maombolezo ,wala kilio..kwa kuwa mambo ya
kwanza yamekwisha kupita ,wala hapana mwenyeji
atakayesema mimi mgonjwa ( UFUNUO 21:4,ISAYA 33:24),(GW 676)
vii.
JE KUMBUKUMBU ZAO ZITAKUWEJE
Kumbukumbu zetu zitakuwa kamili kabisa watu wale walioishi kabla ya gharika walikuwa
hawana vitabu hawakuwa na
kumbukumbu zote zilizoandikwa ,lakini wakiwa wenye nguvu nyingi za kimwili na kiakili ,walikuwa na
kumbukumbu zao thabiti ,zenye uwezo wa kunasa kile walichokuwa wameambiwa ,nao kwa zamu yao kuweza
kuwapa wazao wao bila kuuathiri
ujumbe ule
viii.
JE MACHO YAO YATAKUWA NA UWEZO GANI?
Watakuwa na macho
kama DARUBINI yaonayo vitu vidogo
sana na vile vilivyo mbali sana kwa macho
yaonayo wazi kabisa wataangaza na
kuungalia utukufu wa uumbaji
ix.
JE UWEZO WAO WA KUSAFIRI UTAKUWAJE?
Uwezo wa kusafili katika anga msongamano wa waliokombolewa utazunguka
toka Dunia moja kwenda Dunia nyingine na wakati wao mwingi utatumika katika kuzichunguza siri za ukombozi
x.
JE KUTAKUWA NA MAISHA YA KIFAMILIA, NDOA NA
KUZAA WATOTO KULE?
Hakuna ndoa kule wala kuzaa watoto kuna watu leo wanaoeneza
imani yao wakisema kwamba kutakuwa na ndoa
na kuzaa watoto katika nchi mpya ,lakini basi ,wale wanaoyaamini maandiko hawawezi kulikubali fundisho kama hilo ,fundisho linalosema kwamba
watoto watazaliwa katika nchi mpya
halina sehemu katika lile
neno la unabii lililo imara zaidi (MM99,1SM 172) MATHAYO 22:23-30
xi.
NI KUMBUKUMBU GANI MOJA PEKEE YA KAZI YA
KIKATILI ILIYOFANYWA NA DHAMBI AMBAYO ITAKUWA MBELE DAIMA?
Kumbukummbu moja pekee itabaki: mkombozi wetu daima atachukua
alama zile za kusulubiwa kwake . Juu ya kichwa chake kilichojeruhiwa ,ubavu ni pake ,katika
viganja vyake vya mikono
na miguu ,hizo ndizo alama pekee za kazi
ya kikatili ambayo dhambi
imefanya kwake(gw)
xii.
JE MBINGUNI KUTAKUWA NA IBAADA?-JIBU NDIO
Kukusanyika pamoja kumwabudu Mungu. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na SABATO HATA SABATO, wanadamu wote
watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
xiii.
JE NI
MASOMO YAPI WATAJIFUNZA WATAKATIFU
Baadhi ya masomo
wakayojifunza ni haya watajifunza HISTORIA
YA PAMBANO KUU ,kugundua SABABU YA MATATIZO YOTE YA MAISHA HAYA ,KUJIFUNZA USHINDI WA KILA TENDO JEMA NA
BAYA KATIKA MAISHA HAYA WATATUNGA NYIMBO NA KUSILIZA MUZIKI ULE ULIO MKAMILIFU SANA na mengineyo
MPENDWA USIKOSE jitahidi
ukaone mwenyewe somo linalofuata mji MPYA YERUSALEMU UKISHUKA KUTOKA MBINGUNI
usikose.
No comments:
Post a Comment