Monday, December 19, 2016

MNYAMA WA PILI NI DUBU -S/N 11



 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama DUBU, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele DANIELI 7:5, Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine Mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote DANIELI 2:39

       I.            MNYAMA -Anawakilisha  Ufalme Danieli 7;17

    II.            SIFA YA HUU UTAWALA -Ulikuwa ni ulawala katili sana kwa sababu kosa la mtu mmoja katika familia moja wanahukumiwa wote kuuawa ndio maana unafananishwa na dubu kwa ukatili wake

III.            DUDU NA MADINI YA FEDHA -Yanawakilisha utawala wa  WAMEDI NA WAAJEMI

 IV.            UTAWALA HUU ULINANZA KUTAWALA -Ulimwengu tangu mwaka 538 B.C hadi 331 B.C

    V.            WAFALME WALIOTAWALA HII DOLA -Ni mfalme KORESHI,na DARIO

 VI.            MBAVU TATU KATIKATI YA MENO -Ziliwakilisha majimbo matatu ambayo Wamedi na Waajemi waliyapiga nayo ni  BABELI,LIDIA ,na MISRI

VII.            IFUATAYO NI  HISTORIA FUPI

Enzi  kuu ya pili ulimwenguni

Ufalme huu ulifananishwa katika sanamu  na kifua na mikono ya fedha kama fedha inavyopungua dhamani yake  kuliko dhahabu kadharika wamedi na waajemi ijapokuwa  walikuwa hodari walipungua katika utajiri na utukufu.  

Pia Dubu ni mfano wa ufalme pia kama  Kifua  na  Mikono  ya fedha ya sanamu ,yaani  Umedi na Uajemi kuinuka yenyewe upande mmoja inaonyesha ….Wamedi  chini ya DARIO walikuwa na uwezo mwingi wa kabila zote  mbili mwanzoni  lakini baadaye  waajemi chini ya KORESHI walichua utawala kulikuwa na majimbo matatu yaliyokuwa yameshindwa  ambayo   wamedi  na waajemi waliwafanyia ukatili zaidi baada ya kutokea kwao na  kuwa na mamlaka:BABELI,LIDIA,NA MISRI.hayo yalikuwa mfano wa mbavu tatu katikati ya meno yake hakuna mnyama awezaye  kuwa mkali zaidi kuliko  dubu mwenye  kiu ya damu.ukatili ulikuwa  unaonekana dhahiri  katika tabia ya ufalme  wa waajemi.kama tunavyoona katika sura ya DANIELI 6:24 wake wasiokuwa na hatia  na watoto  wa watu walihukumiwa waliadhibiwa  sawa  nao pamoja nao.

VIII.            Ndugu mpendwa kumbuka zamani walivyokuwa wanahesaba miaka

na mwezi na tarehe  kabla ya kiuzaliwa Yesu walikuwa wanahesabu kurudi nyuma mfano kutoka 2000,1999,600,400,200….lakini baada ya kuzaliwa Yesu tarehe zikaaza kuhesabiwa kwenda mbele badala ya kurudi nyuma,mfano 2000,2001,2003,2004…..

JIANDAE NA SOMO LA TATU LINAHUSU MNYAMA MWENYE VICHWA VINNE AMBAYE NI CHUI

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment