Monday, December 19, 2016

JE UNAMAADUI WANGAPI ?-S/N 8



KAMA JIBU NI NDIYO AU HAPANA ZINGATIA YAFUATAYO .

      I.            CHANZO CHA UADUI NI MAKWAZO YANAYOTOKANA WATU MBALIMBALI

Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.LUKA 17:1-2

   II.            MPENDE ADUI YAKO

Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.MATHAYO 5:43-45, 1 WAKORINTHO13:4-8

 

III.            MWOMBEE ADUI YAKO

lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,  ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.MATHAYO 5:44-45

IV.            USIMFANYIE ADUI YAKO JAMBO BAYA

Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria WARUMI 13:10

   V.            USIWE NA UPENDO WA KINAFIKI AU MCHONGEZI  KWA ADUI YAKO

Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.WARUMI 12:9. Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi Bwana.WALAWI 19:16

VI.            USILIPIZE KISASI WALA KUWA NA KINYONGO

Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake.  Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana WALAWI19:17-18. Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.WARUMI 12:17-19


KANUNI YA MUNGU KWA WALIPA KISASI MITHALI 17:13

Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake

VII.            NAMANA YA KUSHUGHURIKIA MAKWAZO

 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.  Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. MATHAYO 18:15-19

VIII.            USIFURAHI WALA USIKASILIKE ADUI YAKO ANAPOJIKWAA

Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake. Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya; Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika.MITHALI 24:16-20

IX.            UWE TAYARI KUTOA MSAMAHA USIO NA MASHARTI

Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.LUKA 17:3-4.Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?  Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.MATHAYO 18:21-22.Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.MARKO11:25-26

   X.            KUWABARIKI WANAOKUUDHI

Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.WARUMI 12:14

XI.            MHUDUMIE ADUI YAKO

Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.WARUMI 12:20-21.Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.  Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.1 YOHANA 2:?9-11

TAHADHALI kama kuna mtu amekukosea na wewe hutaki kumsamehe na unatunza vinyongo na visasi moyoni mwako ujue kabisa ibaada yako ni   ya bure,maana hata Mungu naye hatakusamehe wewe pia     MARKO 11:25-26 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.  Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment