KATIKA
MAHAKAMA HII KILA MWANADAMU KESI YAKE ITASIKILIZWA NA KISHA KUTOLEWA MAAMUZI.
Somo
hili linavipengele viwili
a.
Kuna maana mbili ya neno hukumu
b.
Hatua nane zinazohusika na mahakama ya mbinguni
A.
KUNA MAANA MBILI ZA NENO HUKUMU
,1
WAKORINTHO 4:5 Basi ninyi msihukumu neno
kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya
giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa
yake kwa Mungu
ANAPOSEMA
MSIHUKUMU ANAMAANISHA NINI - Usijiweke mwenyewe kuwa kipimo cha kuwapimia wengine,
kauli zao, na mawazo yako juu ya mambo yaliyojuu ya mambo yaliyo mujibu,
maelezo yako juu ya neno la Mungu yasiwekwe kuwa kipimo cha kuwakadiria wengine
;tena usiwalaumu wengine moyoni mwako
wakikosa kukifikia kipeo chako AU-Usiwachambue wengine na kuyakisia makusudi yao bila kuyahakikisha na kuwahukumu.
ANAPOSEMA HUKUMU MAANA YAKE NINI?-Ni kutoa maamuzi ya mwisho kwa mtu mhusika kwa uzima wa milele au mauti ya milele
B. HATUA
NANE ZINAZOHUSIKA NA MAHAKAMA
I.
JE
MAHAKAMA HII INAHUSU WATU GANI?
Jibu Mahakama hii inamhusu kila mtu japokuwa
hatutahudhulia kimwli kwenye mahakama hii
2
WAKORINTHO 5:10 Kwa maana imetupasa sisi sote
kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya
mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya
II.
JE NI VITABU GANI HUTUMIWA NA MAHAKAMA HII?
Jibu Mahakama
hii katika kuendesha kesi zake hutumia vitabu viwili tu
KITABU CHA KUMBUKUMBU, MALAKI
3:16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao.
Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele
zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. (Ambacho huandikwa kila
tendo jema na baya ,
KITABU
CHA UZIMA UFUNUO 20:12-15 Tazama, naja upesi, na
ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na
mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao,
wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake Huko nje wako mbwa, na
wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu
apendaye uongo na kuufanya. ( ambacho hutumika kuandika
majina tu ya wale wanaositahili kuokolewa.)
III.
JE NI VITU GANI HUANDIKWA KWENYE HIVYO VITABU?
Jibu ni
mambo mema na mabaya ayafanyayo mwanadu huandikwa kwenye hicho kitabu cha
kumbukumbu MHUBILI 12:14, Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na
kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.MATHAYO 12:36-37 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena
wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako
utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa
IV.
JE KATIKA MAHAKAMA HIYO HAKIMU NA MTETEZI NI
NANI?
Jibu Hakimu na mtetezi
wa hiyo mahakama ni mmoja tu ambaye ni YESU, YOHANA
5:22,26-27 Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali
amempa Mwana hukumu yote; . Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake,
vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. Naye akampa amri ya kufanya hukumu
kwa sababu ni Mwana wa Adamu
V.
JE SHITAKA
AU KESI YA KILA MMOJA HUFUNGULIWA WAKATI GANI?
Jibu Shitaka
au kesi ya kila mmoja hufunguliwa wakati mtu apokufa NDIPO
SHAURI LA MTU HUANZA KUSIKILIZWA MAHAKANI, WAEBRANIA 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya
kufa hukumu
VI.
JE WATU AMBAO WATAKUTWA WAKO HAI WAKATI YESU
ANAPORUDI MARA PILI WAO ITAKUWAJE?
Jibu
watu hawa ni kizazi cha mwisho wao hukumu yao itasomwa wakiwa hai na baada ya
hukumu yao kupita hawataweza kubadilika kama ukiwa mtakatifu utaendelea kuwa
hivyo ,ukiwa mdhambi utaendelea kuwa hivyo,MARKO 9;1 Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa
wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa
Mungu umekuja kwa nguvu,UFUNUO 22:11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na
mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na
mtakatifu na azidi kutakasw
VII.
JE MUNGU ATATUMIA KIGEZO GANI KUWAHUKUMU WATU
Jibu Kigezo
kikubwa kitakachotumika kwenye hii mahakama haijalishi unamwabudu Mungu au
hakuna haijalishi unaenda kanisani au
hakuna kigezo hicho ni SHERI NA INJILI uliyoipokea katika maisha yako WARUMI
2:11-16 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria
watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa
sheria. Kwa sababu sio wale waisikiao sheria
walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa
haki. Kwa maana watu wa Mataifa wasio na
sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria
wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya
torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao,
yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea; katika
siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa
Kristo Yesu
VIII.
JE BAADA YA HUKUMU KUMALIZIKA MAHAKAMANI NINI
KINAFUATA?
Jibu Baada
ya hukumu kumalizika kitakachofuatia ni utekelezaji wa hukumu kwa watakatifu
kupata uzima wa milele na waovu kuchomwa moto UFUNUO 20:5-10. Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka
elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu
katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa
makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu. Na hiyo miaka elfu
itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; naye atatoka
kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu,
kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana
wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka
kutoka mbinguni, ukawala. Na yule Ibilisi, mwenye
kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na
yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
JAMBO
LA KUZINGATIA UNAPOTENDA DHAMBI - huandikwa kwenye kitabu
cha kumbukumbu ukiungama dhambi zote
zinafutwa unaanza tena upya.ISAYA 1:18
haya, njoni, tusemezane, asema bwana. dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana,
zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama
sufu.PIA KUMBUKA UNAPOAMBIWA AU KUFUNDISHWA UKWELI WA NENO LA MUNGU USISEMA UNANIHUKUMU
HUKO SIO KUHUKUMU
.ULIZA SWALI KAMA HAUJAELEWA.
No comments:
Post a Comment