YAFUATAYO
NI MATUKIO YATAKAYOAMBATANA NA UJIO WA YESU ;
I.
JE NI KITU GANI YESU ANASUBULI SASA HIVI?
MATHAYO 24:14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu
wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.kazi
hii itakapomalizika Yesu atarudi mara ya pili
II.
JE
KUTAKUWA NA ISHARA GANI YA KUMTAMBULISHA YESU ANAPOKUJA?
MATHAYO 24:27 Kwa maana Kama vile UMEME utokavyo
mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake
Mwana wa Adamu.
III.
JE NI WINGU GANI LITAONEKANA KAMA UTAMBULISHO WA
MFALME WA WAFALME?
Wingu
dogo jeusi litaonekana upande wa mashariki.Mfalme wa wafalme atashuka na wingu
lililozungushiwa moto unaowaka .dunia
itatetemeka mbele yake “Mungu wetu atakuja
wala hatanyamaza moto utakula
mbele zake na tufani
yavuma sana ikimzunguka pande
zote . Ataziita mbingu zilizo juu na nchi pia awahukumu watu wake ZABURI
50:3-4
IV.
JE KUTAKUWA NA MAKUNDI MANGAPI YATAKAYOMUONA
YESU ANAPORUDI?
Ufunuo
1:7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho
litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili
yake. Naam. Amina. KUTAKUWA
NA MAKUNDI MATATU WATAKAOMWONA BWANA Kundi la kwanza ni laWafu
waliolala katika Bwana au katika tumaini la kumlaki Kristo.Kundi la pili Watu waaminifu
watakaokutwa wako hai juu ya uso wa nchi.Kundi la Tatu ni la watu maalumu la
wenye dhambi hasa walimsulubisha pale msalabani watafufuliwa ili wamwone Yesu
washuhudie maana aliwaahidi hili kundi
likiisha kumwona wote watakufa tena MATHAYO
26:64
V.
JE KUTAKUWEPO NA TETEMEKO LENYE KIWANGO GANI
YESU ANAPORUDI?
Kutakuwepo
na Tetemeko kubwa ambalo halijawahi kutokea katika historia ya mwanadamu UFUNUO
16:18
Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko
la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile,
jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
VI.
JE NI
MAKUNDI MANGAPI YATAKAYOFUFULIWA WAKATI YESU ANAPORUDI?
1 WATHESALONOKE
4:13-18. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka
kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya
Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai,
tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani;
na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
KUTAKUWA NA MAKUNDI MAWILI
KUNDI LA KWANZA ni
la watu waliokufa nalo limegawannyika mara mbili moja ni KUNDI
LA WAFU WALILALA KATIKA BWANA TU,kundi la
pili ni KUNDI MAALUMU LA WENYE DHAMBI hasa ambao walimsulubisha Yesu msalabani MATHAYO 26:64
ambao ni Herode,watu waliomvika taji ya miiba, wale walisujudu mbele yake kwa
dhihaka ya kukufuru,wale waliomtemea mate,wale waliompigilia misumari.hawa ndio
watakaofufuliwa, kundi hili la waovu watakufa mara tatu yaani sasa hivi
wameshakufa,Yesu anaporudi mara ya pili wafufuliwa kisha watakufa ,kwenye
ufufuo wa pili wa waovu watafufuliwa tena kisha watachomwa moto pamoja na waovu wengine
KUNDI LA PILI ni la
watu watakaokutwa wako hai nalo limegawanyika mara mbili moja ni watu wakakatifu ambao wataungana na wafu
waliolala katika Bwana watakaofufuliwa
kisha watamraki Bwana mawinguni,kundi la pili ni watu waovu watakaokuwa hai
hawa watamuona Yesu kisha watakufa UFUNUO 20:5
VII.
JE SANAMU
AMBAZO LEO WANADAMU WANAZIABUDU ZITAWEZA KUWAOKOA ?
ISAYA
2:18-21 Nazo sanamu zitatoweka kabisa. Na watu
wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za
utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno
dunia.Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu
zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo;
VIII.
JE
MBINGU HIZI TUNAZOZIONA ZITAKUWEJE WAKATI YESU ANAPOKUJA?
UFUNUO 6;16 Mbingu zikaondolewa
kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali
pake
IX.
JE KUNA
UNYAKUO WA SIRI? JIBU HAPANA
MATHAYO 24:40-41 Wakati
ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake
wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.FUNGU hili
halimaanishi eti kutakuwa na unyakuo wa siri kwamba unashutukia tu
mwenzako hayupo tayari ameenda mbinguni
hilo ni fundisho potofu Yesu anaporudi kila jicho litamwona.fungu hili
humaanisha kuwa swala la wokovu ni la kila mmoja hatutaenda mbinguni kama
familia,marafiki,kanisa bali kila mmoja atasimama peke yake.
MPENDWA USIKOSE SOMO LINALOFUATA AMBALO LINASEMA KIFUNGO CHA SHETANI CHA MIAKA
1000
UKIWA NA SWALI ULIZA
,
No comments:
Post a Comment