Monday, December 26, 2016

JIFUNZE UNABII WA MAJUMA SABINI;S/N 15


Muda wa majuma sabini  umeamriwa juu ya watu wako  na juu ya mji wako  mtakatifu ili kukomesha  makosa ,na kushiliza dhambi ,na kufanya upatanisho kwa ajiri ya uovu , na kuleta haki ya milele ,na kutia muhuri  maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu . DANIELI 9:24-27
MALENGO SITA YA MAJUMA SABINI
HUELEZEA KIMSINGI KILE KITAKACHOKAMILISHWA NA MAISHA NA HUDUMA YA KRISTO HAPA DUNIANI.
1)   KUKOMESHA MAKOSA- HUMAANISHA
Makosa kuhusu uvunjaji wa mahusiano baina ya Mungu na mwanadamu, Kwa njia ya kafara yake pale msalabani. Yesu aliunganisha tena uhusiano uliokuwa umevunjika na kutulejesha kwa Yesu
2)   KUISHIRIZA DHAMBI-HUMAANISHA
Gabriel hapa anatangaza  kuwa  masihi  ataushugulikia udhaifu wa mwanadamu ,atazibeba  dhambi  zao  na hivyo  kuziiishiliza( KUZIKOMESHA)
3)   KUFANYA UPATANISHO KWA AJIRI YA UOVU-HUMAANISHA
Uovu ni dhambi kama ukiukaji walililosahihi kupitia kafara yake ya upatanisho pale msalabani Yesu Kristo alishugulikia dhambi katika kila nyanja yake.
4)   KULETA HAKI YA MILELE-HUMAANISHA
Kupitia anguko  wanadamu  wamepotoka  na  wasio  haki  masihi aeleza Gabriel ataleta haki kutoka kwa Mungu ambayo itakuwa  ni ya milele  kwa wote ambao huidai haki hii kuwa yao kwa njia ya imani iongozayo katika utii.
5)    KUTIA MUHURI MAONO NA UNABII-HUMAANISHA
Wazo la kutia muhuli hapa  halikuhusu  kufunga bali kuthibitisha  kuidhinisha “ utimizo wa unabii kuhusu kuwasili kwa msihii katika muda maalumu uliotajwa katika unabii  huu  hutupatia  uthibitivu kwamba mambo mengine  yaliyotabiliwa katika unabii hasa hasa huo wa siku 2300 hakika utatimia  kama ilivyotabiliwa .
6)   KUMTIA MAFUTA YEYE ALIYE MTAKATIFU MNO -HUMAANISHA
Mahekalu yalikuwa yanawekwa  wakfu ili  kuzindua  huduma zake(  kutoka 40:9) uwekwaji wakfu  wa huduma  ya Kikuhani ya kristo katika  hekalu la mbinguni baada ya  kupaa kwake WAEBRANIA 9:21
 
FAFANUZI zaidi jina GABRIELI maana yake katika kiebrania  ni  nguvu ya MUNGU  au mtu wa MUNGU
 
Naomba usikose masomo yanayofuata yanayohusu unabii huu wa majuma sabini  somo linalofuata linasema NYAKATI MBILI KUANZA PAMOJA


 

 

 

No comments:

Post a Comment