MAANA
YA MAJARIBU-Majaribu ni mvuto na ushawishi kufanya dhambi,nayo hayatoki kwa Mungu ,bali kwa shetani na kwenye
uovu wa moyoni mwetu sisi wenyewe.Mungu hawezi kujaribiwa na maovu,wala
yeye mwenyewe hamjaribu mtu. YAKOBO 1:13
JIFUNZE
MAMBO TISA YANAYOELEZA UKWELI ULIVYO:
I.
CHANZO KIKUBWA CHA MAJARIBU HUSABABISHWA NA
TAMAA ZETU.
Mtu
ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na
maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku
akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua
mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti: YAKOBO
1:13-15
DHIKI
KUU INAKUJA LAKINI KUNA TUMAINI SURA YA 17, UK, 141
Jaribu
lenye nguvu kushinda yote halimpi mtu kisingizio chochote cha
kutenda dhambi .haidhuru shinikizo linalowekwa juu ya mtu
liwe kubwa kiasi gani ,uasi ni tendo
letu wenyewe.Haimo katika uwezo wa dunia wala wa jehanamu kumlazimisha
mtu ye yote kutenda dhambi ,nia ya mtu ni lazima ikubali ,Moyo wake ni
lazima ukubali kutii ,ama sivyo tama ya
mwili haiwezi kutawala
akili ,wala uovu kuishinda haki
II.
KILA MMOJA ATAJARIBIWA .
Lakini
kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa
utukufu wake mfurahi kwa shangwe.Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri
yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. Maana mtu wa kwenu
asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na
mambo ya watu wengine. Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali
amtukuze Mungu katika jina HILO 1 PETRO 4:13-16,(1
Petro2:21,1:6-7,Waebrania 12:11 )
MLIMA
WA BALAKA SURA YA 2, UK 47
(Heri
wenye kuudhiwa kwa ajiri ya haki maana ufalme wa mbinguni ni wao)
Kama
wanadamu wakijaribu kupatana na Mungu
wataona kwamba chuki ya msalaba
haijabadilika ,Falme na mamlaka
na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho hushindana
nao wote wanaojitoa kuitii sheria
itokayo juu ,kwa hiyo badala ya
kuhuzunika kwa sababu ya mateso ,INAWAPASA WAFUASI WA KRISTO KUYAFURAHIA MATESO ,kwani ndiyo yanayoshuhudia ya kwamba wanazifuata nyao za
Bwana wao.
III.
ILI UITWE MSHINDI UTAPITIA MAJARIBU MENGI.
Wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae
katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa
njia ya dhiki nyingi MATENDO 14:22 :Wapenzi msione kuwa ni ajabu
ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu kana kwamba ni
kitu kigeni kiwapatacho. 1 PETRO 4:12
IV.
KUSTAHIMILI MAJARIBU
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha
kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. Yakobo 1:12, Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia
katika majaribu mbalimbali;
mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na
iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na
neno:YAKOBO 1:2-4,
V.
KUMBUKA
CHANGAMOTO UNAYOPITIA NI YA MUDA KITAMBO TU
Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje
unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. 2 WAKORINTHO 4:16-18
Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. 2 WAKORINTHO 4:16-18
MLIMA
WA BALAKA SURA YA 2,UK 48
(Heri
wenye kuudhiwa kwa ajiri ya haki maana ufalme wa mbinguni ni wao)
Kwa
njia ya majaribu na mateso, tabia –YAANI SIFA YA MUNGU
hufunuliwa kwa wateule wake . Watu kama kanisa la Mungu ambao huchukiwa na
kuteswa walimwengu huwa wakielimishwa na
kuadilishwa katika skuli ya
kristo.hufuata njia nyembamba duniani;hutakaswa katika moto wa mateso.humfuta
kristo katika mashindano makali
hustahimilin katika kujinyima na
kudhihakiwa lakini katika maumivu ya
mambo yanayowapata watu wa Mungu hujifunza
hatia na uovu wa dhambi jinsi ulivyo na jinsi unavyoleta huzuni ,nao
huichukia sana dhambi wakishiriki mateso
ya kristo ndivyo watakavyokuwa washiriki wa utukufu wake.
VI.
MUNGU AMEANDAA MLANGO WA KUSHINDA CHANGAMOTO.
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya
wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo;
lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze
kustahimili 1 WAKORINTHO 10:13
VII.
ILI USHINDE JARIBU NI LAZIMA UWE NA IMANI
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye
akisita-sita, roho yangu haina furaha naye: WAEBRANIA 10:38
MAANDIKO YA AWALI AU EARLY WRITING
SURA YA 8 UK 41: JARIBIO LA IMANI YETU
Katika wakati huu wa kujaribiwa sisi
tunahitaji kutiana moyo na kufarijiana .majaribu ya sheteni kwa sasa ni mengi zaidi kuliko ilivyowahihi
kuwepo, maana anajua kwamba muda wake ni
mfupi na kitambo kila kesi itakuwa imeamuriwa aidha kwa uzima au kifo .huu si wakati wa kuzama
katika hali ya kukata tamaa na majaribu:tunapaswa kuvumilia yote yanayotuumiza
na kutumainia kabisa nguvu zake
Mungu kabisa ,tunaweza kushinda kila
jaribu na kupata ushindi kupitia neema yake.
SURA YA 8 UK 42: JARIBIO LA IMANI YETU
MUNGU amenionyesha kuwa yeye huwapa watu wake kukinywea
kikombe kichungu ili kuwasafisha na kuwatakasa .ni kikombe kichungu ,lakini nao
wanaweza kukifanya kiwe kichungu zaidi na zaidi
kwa kulalamika na kunungunika na kuona
uchungu.na wale wanaokipokea
kikombe hicho kwa malalamiko na
manunguniko inalazimika wapate kikombe
kingine maana kile cha kwanza
hakijafanya makusudi yake moyoni
.na kama kile cha pili hakitafaulu,atalazimika kupata kingine na kingine .baada ya kingine mpaka makusudi
ya Mungu yafanyike ama siyo
wataachwa kuwa wachafu na moyo usiotakaswa.niliona kuwa kikombe
hiki kichungu kinaweza
kufanywa kuwa kitamu kwa uvumilivu
ustahimilivu na maombi.na kwamba
kitafanya makusudi yake kwa wale wote wanaokipokea kwa namna hiyo ,na Mungu
ataheshimiwa na kutukuzwa.
VIII.
LENGO KUBWA LA
MAJARIBU NI KUKUTAKASA DHAMBI:
...... ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko
dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye
sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo 1 PETRO 1
:6-7
TUMAINI
KUU, UK 324, SURA 32
(Kinasema
namna ya kumshinda shetani/ushindi wa kutosha uk 325.)
BWANA
anaruhusu watu wake wapate majaribu makali siyo kwa sababu anaifurahia dhiki
yao lakini kwa ajili ya utukufu wake hawezi kuwakinga na majaribu kwani lengo
la majaribu ni kuwatayarisha kwa ajili ya kuvipinga vivutio vyote vya uovu.
Watu
waovu na mashetani hawawezi kuuondoa
uwepo wa Mungu katoka kwa watu wake endapo wataungana na kuziweka mbali dhambi zao na kuzidai ahadi zake kila
jaribu la wazi ama siri linaweza kupingwa
kwa mafanikio si kwa nguvu bali ni kwa roho yangu asema BWANA WA
MAJESHI.
KITABU
CHA PAMBANO KUU
SURA YA
30, UK 130 (shetani
apigana na binadamu)
Kama
tukiletwa katika majaribu tutakuwa na hakika kuwa Mungu atatulinda, lakini
tukijipeleka wenyewe majaribuni tutaanguka tu bila shaka.
IX.
JE MUNGU ANAPENDA AU ANAFURAHI WATU WAKE WAPATE MATESO?
MAOMBOLEZO
3:33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha
MLIMA
WA BALAKA SURA YA 2 UK 25-27
(Heri
wenye huzuni maana hao watafarijika)
Hatupati
mateso bila sababu ,kwani Mungu moyo
wake hapendi kuwatesa wanadamu ,Wala kuwahuzunisha.Mungu anaporuhusu
tupatwe na majaribu na taabu ,Sababu yake ni kwa faida
yetu ili tuushiriki utukufu wake(WAEBRANIA
12;10)
LILE
JARIBU LINALODHANIWA KUWA NI UCHUNGU NA GUMU KULIVUMILIA ,LIKIPOKELEWA KWA IMANI INAONEKANA KUWA NI MBARAKA ,Lile pigo
kali linalozimisha furaha za Dunia
litakuwa njia ya kuyageuza macho
yetu kuangalia juu mbinguni .ni wengi ambao wasingelimjua
YESU isipokuwa misiba
imewaongoza kutaka kufarijiwa naye
Taabu
maishani ni kama watenda kazi wa Mungu
kwa kutoa uchafu na mambo yaliyo
maovu katika tabia zetu
na kutukamilisha tuwe na sifa
njema .katika kuchongwa kukatwa na kukwatuliwa yapatikana maumivu –kukandamizwa kwa jiwe la kunolea ,lakini Yule avumiliaye katika
majaribu mwishowe atafanywa
kuwa kama jiwe zuri la jingo la
Mungu .Bwana hatendi kazi nyingi kwa
bidii hivi kwa kitu kisichofaa ili kwa vito vyake vya dhamani
tu vinavyonakishiwa vifae kwa jingo la
hekalu
Lakini
tukipatwa na shida ,wengi wetu hufanana
Yakobo.tunafikiri kuwa ni mkono
wa adui ulio juu yetu nasi tunashindana gizani hata nguvu zetu
zimekwisha ,bila bila kusaidiwa wala kukombelewa ,yakobo alipoguswa wakati
wa mapambazuko akaona kumbe
Yule aliyeshindana naye ni
malaika wa Mungu naye Yakobo
alipoona hana nguvu akajitupa mbele yake apate mbaraka alioutamani kupata moyoni
mwake ,Hata nasi pia inatubidi kujifunza kuwa majaribu yaweza kuwa nafuu kwetu ,tusidharau kurudi kwake Bwana
,wala tusizimie moyo tukikemewa naye (WAEBRANIA 12:5)
ULIZA
SWALI KAMA HAUJAELEWA
No comments:
Post a Comment