MAMBO MANNE TUNAYOJIFUNZA
I.
ILI UPOKEE BARAKA AU UBARIKIWE NI LAZIMA UFANYE
JAMBO MOJA TU AMBALO NI KUTII
TORATI 28:1
Itakuwa utakaposikia sauti
ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote
nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako,atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya
duniani;
II.
IFUATAYO NI ORODHA YA BARAKA KAMA MATOKEO YA
UTII
TORATI 28:2-14
Na baraka hizi zote
zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.Utabarikiwa mjini,
utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa
nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na
wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia
unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. Bwana atawafanya adui zako
wainukao juu yako kupigwa mbele yako; ..................
III.
TAHADHALI UKIBARIKIWA USIFANYE JAMBO HILI
TORATI 8:11-14,17 1
Jihadhari, usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa
kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. Angalia,
utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng'ombe na kondoo
yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu
ulicho nacho kitakapoongezeka;basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana,
Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;
IV.
MUNGU HUTOA ADHABU KWA WALE WANAOTUMIA VIBAYA
MIBARAKA YAKE.
MFANO MFALME
NEBUKADREZA-kosa alilolifanya alijiinua na kujisifu aliadhibiwa kuwa
mnyama na kula nyasi kwa miaka saba DANIELI 4:28-32 Hayo yote
yakampata mfalme Nebukadreza. Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea
ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio
Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu
zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu? Hata
neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni,
ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu
umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na
wanadamu, ............ (,MITHALI
16:18)
MFANO MFALME HERODE-kosa alilolifanya
hakumpa Mungu utukufu; MATENDO 12:20-23 Naye Herode alikuwa amewakasirikia sana watu wa Tiro na
Sidoni; ....... Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi,
akatoa hotuba mbele yao. Watu
wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu. Mara
malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango,
akatokwa na roho.
MFANO MFALME SULEMANI-kosa
alilolifanya alijitukuza na kutegemea hekima yake,kuabudu miungu,kuoa wake
zaidi ya mmoja Mungu alimwondolea ulinzi wake na maadui zake wakaanza kumshambulia pande
zote 1 WAFALME 11:14-28 Ndipo Bwana akamwondokeshea Sulemani adui, Hadadi
Mwedomi; yeye alikuwa wa wazao wake mfalme wa Edomu.
USIPOTII MAAGIZO YA MUNGU
BARAKA ZOTE ULIZOPEWA NA MUNGU ZINAGEUKA KUWA LAANA
TORATI 28:15-29 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu
wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi
leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini,
utalaaniwa na mashambani. Litalaaniwa
kapu lako na chombo chako cha kukandia.Utalaaniwa uzao wa tumbo lako,
................
WITO ,YEREMIA 9:23-24:Bwana asema hivi, Mwenye hekima
asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya
nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye na
ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni
Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa
na mambo hayo, asema Bwana
No comments:
Post a Comment