Monday, December 26, 2016

UNABII WA MUHURI SABA NI SAWA NA UNABII WA MAKANISA ;S/N 23


UFUATAO NI MCHANGANUO WAKE

UFUNUO 6:1 Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri Saba, nikasikia mmoja WA wale wenye uhai wanne akisema, Kama Kwa sauti ya ngurumo, Njoo

JE MUHURI SABA INAWAKILISHA NINI?-MUHURI SABA Inatuleta ama katika ushindi wenye utukufu au katika kushindwa kunakotisha katika ibaada ya utukufu ya kuja kwa YESU.

JE FARASI HUWAKILISHA NINI?- FARASI NI mfano wa wajumbe wa MUNGU wajumbe waliotumwa kuleta vyote wokovu na hukumu.

MUHURI WA KWANZA.(kanisa la Efeso)

 FARASI MWEUPE.

UFUNUO 6:2 Nikaona, Na tazama, farasi mweupe, Na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda

MAANA YA KWANZA YA FARASI MWEUPE-Farasi mweupe Ni mfano wa kuhesabiwa haki na ushindi.

MAANA YA PILI YA FARASI MWEUPE-Farasi mweupe Ni barabara ya kufaulu injili katika karne ya kwanza ya historia ya Ukristo, hii ilikuwa mfano wa kanisa la Mitume sawa na MFANO WA KANISA LA EFESO katika Ufunuo 2:1

UTA UNAMAANISHA NINI?-Uta katika mkono ni uhakikisho wa ROHO Mtakatifu katika mioyo ya wanadamu.Maneno ya mitume yalikuwa makali Kama mishale ya Mwenyezi yakithibitishia wadhambi uovu wa kutisha katika kukataa na kumsubisha Bwana wa utukufu.

MUHURI WA PILI (kanisa Smirna)

FARASI MWEKUNDU.

UFUNUO 6:3-4 Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo!  Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa

FARASI MWEKUNDU HUWAKILISHA NINI ?–Ni mfano wa mauaji na mateso waliofanyiwa wafuasi wa YESU baada ya wakati wa Mitume ambacho ndicho kipindi cha KANISA LA SMIRNA KATIKA UFUNUO 2:8

MUHURI WA TATU.( kanisa la pergamo)

FARASI MWEUSI

UFUNUO 6:5-6 Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai

FARASI MWEUSI  ALIWAKILISHA NINI?-Aliwakilisha hali za watu wa MUNGU zilikuwa zinaendelea kuwa ngumu kwanza .FARASI MZURI MWEUPE akiwa mfano wa usafi  na ushindi halafu MWEKUNDU sana ni mfano wa mateso  na kisha sasa mfano wa kutisha wa njaa( farasi huyu MWEUSI nawakilisha  kuwa ne no la Mungu liliadimika siku  hizo za kanisa la pergamo)

SAUTI ILIYOTANGAZA HABARI MBAYA  kibaba cha ngano au shayiri kilikuwa ndicho posho ya kila kila siku kama vile ratili moja na nusu ya unga  wa mahindi wakati mwingine unafikiliwa  kilikuwa chakula cha kila siku cha askari wa kiafrika.RUPIA katika nyakati za agano jipya  ilikuwa ndiyo ujira wa kibarua kwa siku nzima (Mathayo 20:1,20)

PERGAMO CHA UFUNUO 2:12 Hekaya za kupendeza na mapokeo ya wanadamu yalilisonga mno neno la Mungu wale waliokwenda kanisani walipata chakula haba cha kulisha roho zao

Nakala za biblia zikawa adimu kiasi kidogo tu cha neno la MUNGU kikawa na thamani kama chakula kidogo wakati wa njaa

MUHURI WA NNE (kanisa la Thiatira)

FARASI WA RANGI YA KIJIVUJIVU

 UFUNUO 6:7-8 Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.

RANGI YA KIJIVUJIVU HUWAKILISHA NINI?-Rangi hii inaonyesha rangi ya mauti yenyewe.wanafunzi wa biblia  wameelewa kwa miaka mingi kuwa farasi wa nne  maana ya hali ya UFU YA KANISA la(zama za kati) wakati  kati ya mwaka 538 BK mpaka wakati matengenezo ya Kiprotestanti wakati ambapo kanisa liliokolewa sehemu tu kutoka nguvu  za UPAPA.

ROHO YA NCHI HUWAKILISHA NINI?-Robo ya nchi itakuwa basi na maana ya sehemu ya nchi ya mateso ya MAMILLIONI YA MASHAIDI WA WAKATI WA ZAMA ZA GIZA (538 BK-1517 BK)

MUHURI WA TANO.(kanisa la sardi)

UFUNUO 6:9-11 Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?  Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao

NGUO NDEFU HUWAKILISHA NINI?-Kwa kawaida inaeleweka kwamba maneno NGUO NDEFU nyeupe huwakilisha heshima Kwa Mashahidi Waliokufa Kama KAFARA YA UPAPA.

MFANO WA WATU WALIOVIKWA NGUO NDEFU NYEUPE -Kwa maana ya kwanza watu Kama WYCLIFFE.HUSS NA JEROME walikuwa wamechukiwa na UPAPA walipewa heshima kuwa watumishi wa kweli wa Mungu. KIPINDI HIKI KILIANZA (1517-1798)

MUHURI WA SITA.(kanisa la Filadelfia)

UFUNUO 6:12-17 Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

MUHURI WA SITA ULIANZA (1798 A.D-1844 A.D)`Nyakati za zama za giza sasa zimekwisha pita na matukio makubwa yanaanza kutokea duniani .

KULITOKEA NA MATUKIO KAMA YAFUATAYO MOJA

TUKIO LA KWANZA LA TETEMEKO-Tetemeko kuu ambalo halijawahi kutokea mnamo asubuhi ya Novemba 1, 1755. karibu WATU 30,000 waliuawa katika muda wa DAKIKA SITA.

TUKIO LA PILI LA GIZA - -Tukio kubwa lilifuatia miaka michache baadaye siku ya Mei 19, 1780 siku ya kiza.

TUKIO LA TATU LA KUUNGUKA KWA NYOTA LILIFUATA-Nyota za mbinguni zikaanguka juu ya nchi Kama vile mti upukutishavyo mapooza yake Novemba 13.1833.

MUHURI YA SABA. ( kanisa la laodikia)

UFUNUO 8:1 Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba.  Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.

NINI KINACHOLETA KIMYA HIYO?-sura ya saba imetupwa kati  ya sura ya kufungua muhuri ya sita  tuliona waovu  wakiiambia miamba  na milima iwaangukie  na kuwasitiri mbele za uso  wake  yeye  aketiye juu ya kiti cha enzi na hasira  ya mwana kondoo

Mamia ya wengi wa wakaaji wa Dunia wameukataa msalaba na wamechagua kuangamia na hivyo wakati wakiangamia kuna kuwa kimya mbinguni

MUDA HUU WA NUSU SAA HUWALIKISHA NINI?- Nikipindi cha unabii ambacho siku ni sawa na mwaka mmoja basi kimya kitachukua kama juma moja.

UNABII WA MAKANISA SABA ;S/N 22

UFUATAO NI MCHANGANUO WA KANISA  MOJA  HADI JINGINE.

UFUNUO 1:3-4,20 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

KANISA LA KWANZA LA EFESO;

      I.            JE MAKANISA SABA YANAMAANISHA NINI?

MAANA YA KWANZA YA MAKANISA SABA- Majina ya makanisa Saba ni mfano wa kanisa katika zama mbalimbali za kikristo

MAANA YA PILI YA MAKANISA SABA-Ni mifano iliyotumiwa huonyesha hali ya kanisa Kwa nyakati tofauti katika historia ya ulimwengu.

MAANA YA TATU YA MAKANISA SABA- Makanisa saba yanasimama badala ya kanisa  zima  kwa wakati wote  wa historia  yake tangu  nyakati za mitume  hadi  siku za mwisho kabla ya YESU kurudi mara ya pili .

   II.            JE MALAIKA SABA HUWAKILISHA NINI? - Ni “wajumbe au“uongozi wa kibinadamu wa kanisa katika kila kipindi Mungu huzungumza na watu wake kupitia watumishi wake aliowateua

III.            JE KANISA LA KWANZA NI LIPI-KANISA LA KWANZA NI LA EFESO.

UFUNUO 2:1, 7 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu

IV.            JE KANISA LA EFESO LINAMAANISAHA NINI? –Linamaana ya tamaniao au kupendeza

   V.            JE KILIKUWA NI KIPINDI CHA KINANANI?-

Kilikuwa kipindi cha mitume (kanisa) walipeleka habali njema ya wokovu Kwa ulimwengu wote,

VI.            JE KIPINDI CHA KANISA HILI KILIANZA WAKATI GANI?

Muda wa kanisa la EFESO ni kuanzia 31 A.D-100 AD


KANISA LA PILI SMIRNA

UFUNUO 2:8-11 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

             i.            JE KANISA AU NENO SMIRNA HUMAANISHA NINI?-Neno Smirna linamaanisha kitu kilichoinuka vizuri.Hiki ni kipindi cha pili cha kanisa kilikuwa kimojawapo cha mateso na maumivu

           ii.            JE KIPINDI CHA KANISA LA SMIRNA KILIANZA WAKATI GANI?-Muda wakanisa la Smirna kilianza karibu na 100AD-313AD

 

        iii.            JE SINAGOGI LA SHETANI WALIKUWA WAKINANI?-Sinagogi la Shetani –Huenda walikuwani Wayahudi wa siku zile ambao mara kwa mara waliwatesa wafuasi wa awali wa YESU.WARUMI 2:28-29

         iv.            JE SIKU KUMI ZA MATESO ZILICHUKUA MUDA GANI?- Siku kumi za za mateso Ni kipindi katika muda wa unabii.siku moja husimama Kwa mwaka HESABU 14:34, EZEKIELI 4:6 kwa hiyo siku kumi za mateso ni miaka kumi ya MATESO YA KISHENZI makali na ya mwisho yalikuwa chini ya mfalme DIOCLETIAN kati ya mwaka 303 A.D -313 A.D

 

KANISA LA TATU PERGAMO

UFUNUO 2:12-17 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.  Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.  Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.  Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.  Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

a.     JE KANISA AU NENO PERGAMO HUMAANISHA NINI? –humaanisha mwinuko, kimo, urefu

b.   JE KIPINDI HIKI CHA KANISA KILIANZA LINI?-Kipindi cha kanisa la Pergamo kuianza mwaka kati ya 313 A.D-538 A.D. huu ulikuwa wakati ambao mateso yalikoma kabisa na hata mfalme Konstantino mwenyewe alijifanya kuwa Mkristo.

c.     JE ANTIPA NI WAKINANI?-Kanisa lilitukuzwa na kusifiwa liliingia katika wakati wa hatari kubwa .Historia haitufahamishi Mtu yoyote aliyeitwa antipa lakini inaeleweka kuwa jina hili ni mfano wa kikundi cha watu katika kanisa waliopoteza maisha yao Kwa sababu ya kuitetea kweli ya Mungu dhidi ya kiburi cha Mapapa wa Rumi

ANTI -Maana yake ni kupinga PA -inamaana ya baba au Papa (pope) hivyo ANTIPA walikuwa ni wale waliopinga kukua kwa uwezo na madai ya upapa (papacy)  .


KANISA LA NNE THIATIRA

 (NI MWENDELEZO WA MAKANISA SABA)

UFUNUO 2:18-20 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.

JE JINA THIATIRA LINAMAANISHA NINI?-Thiatira inamaana ya kafara na toba

JE KIPINDI HIKI KILIANZA WAKATI GANI?-Kilikuwa nikipindi cha Zama za Giza kilianza MWAKA 538 A .D-1517 A.D (maelezo zaidi soma somo linalosema ZAMA ZA GIZA)

 

KANISA LA TANO SARDI

UFUNUO 3:1-2 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.  Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.

JE JINA SARDI LINAMAANISHA NINI–linamaanisha kanisa la Waprotestanti Wanamatengenezo?

JE KANISA HILI LA SARDI LILIANZA WAKATI GANI?- Tunaweza kuelewa kipindi hiki   kuwa ni kuanzia yapata mwaka 1517-1798 A.D Wakati MARTINI LURTHER HADI KUFIKIA 1798

JE NI WATU GANI WASIOYATIA UCHAFU MAVAZI YAO?- Watu Wasioyatia mavazi yao uchafu wanaweza kutajwa wacha Mungu waadilifu Kama LUTHER, COUNT NZINZENDORF, WESLEY, WHITEFIELD NA WENGINE.

 

KANISA LA SITA FILADELFIA

UFUNUO 3:7-8-13 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.  Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.  Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa

JE NENO FILADELFIA HUMAANISHA ninI? -FILADELFIA humaanisha upendo wa kindugu/ndugu,Hii ndio roho iliyolienea kanisa mwanzoni mwa nyakati za mwisho.

JE KANISA HILI LILIANZA WAKATI GANI? -Kipindi hiki kilianzia mnamo 1798 A.D- 1844 A.D.popote katika ulimwengu wakristo kanisa lilifurahishwa na maandiko na mwamko waajabu, vyama vya BIBLIA vilianzishwa na maandiko na maandiko yalizidi kuongezeka.

Kwa mara ya kwanza watu walianza Kwa dhati kujifunza vitabu vya DANIELI NA UFUNUO

KANISA LA SABA LAODIKIA

UFUNUO 3:14-22 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.  Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.  Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.  Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

JE NENO LAODIKIA LINAMAANISHA NINI? Laodikia maana yake ni kuwahukumu watu.

KANISA hili linaishi duniani wakati wa kuhubiliwa kwa ujumbe wa malaika wa kwanza UFUNGUO 14:7

Tangu Yesu alipoanza kazi hii ya hukumu au kutakaswa kwa PATAKATIFU mwaka 1844 alipoingia sehemu ya pili na ya mwisho ya yake danieli 8:14 tunaelewa kuwa kanisa la laodikia litachukua kipindi cha kuanzia 1844 mpaka MWISHO WA HISTORIA YA MWANADAMU WAKATI YESU AKAPORUDI MARA YA PILI.

MPENDWA SOMO LINALOFUATA  NI  UNABII  WA  MUHURI SABA USIKOSE..

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

YERUSALEMU MPYA UKISHUKA KUTOKA MBINGUNI;S/N 21



UFUNUO 21:1-2 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe

      I.            Angalia jinsi mji mtakatifu Yerusalemu ulivyo jengwa na unavyoonekana.

UFUNUO 21:10- 21   10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu; wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu. Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.  Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.  Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika. Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.  Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto. Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

II.            kuna masharti  mawili  ya huu  mji mtakatifu   

Moja hauhitaji jua wala mwezi ili kuuangaza mbili milango yake haitafungwa kamwe UFUNUO 21:23,25    Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. . Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.    

III.            Historia fupi baada ya miaka 1000 kumalizika.

Mwisho wa miaka 1000 kristo  atarudi  Duniani  akisindikizwa na waliokombolewa na jeshi la malaika ,Atawaamuru waovu waliokufa   kufufuka  ili wapokee hukumu yao.Watafufuka  watakuwa hawahesabiki  kama mchanga wa bahari ,wakiwa na dalili za ugonjwa na mauti .tofauti ilioje  baina ya wale waliofufuliwa  kwenye ufufuo wa kwanza

Kila  jicho  litakuwa  limegeuka  kuutazama utukufu wa Mwana  wa Mungu  kwa sauti  moja jeshi la waovu litasema : amebarikiwa  yeye ajaye  kwa jina la Bwana  MATHAYO 23:39 si upendo  utakaosababisha  tamko hili ,nguvu ya ukweli  italazimisha maneno  kutoka kwenye midomo   isiyoradhi kutamka kama ilivyokuwa  wakati walipolala katika  makaburi yao ,waovu watafufuliwa wakiwa na uadui ule ule  kwa  Kristo wakiwa  na roho ile ile ya uasi .hawatapata kipindi kingine  cha rehema  ili kurekebisha maisha yao yaliyopita

Nabii anasema “Miguu yake   itasimama juu ya mlima  wa MIZEITUNI nao mlima wa mizeituni utapasuka  katikati yake  ZEKARIA 14:4 Yerusalemu Mpya  utakaposhuka kutoka mbinguni , utakaa juu ya mahali palipotayarishwana Kristo na waytu wake  na malaika  wataingia kwenye Mji Mtakatifu 

Akiwa amekatiliwa mbali  na kazi  za udanganyifu ,mkuu wa uovu  atakuwa  na huzuni  na kuvunjika matumaini ,lakini waovu waliokufa  watakapofufuliwa  na atakapouona mkutano  mkubwa  ukiwa upande wake ,Matumaini  yake yatakuwa hai .hakusudii kushindwa  katika pambano kuu .atawapanga waliopotea chini ya bendela yake. kwa kumkataa Kristo  waliukubali utawala wa mwasi ,walikuwa tayari kutimiza amri zake.akiwa bado na hila zake  za awali . atakataa kukiri kuwa yeye ni shetani ,atadai kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa Dunia ambaye urithi wake ulinyanganywa pasipo  uhalali.atajionyesha mwenyewe kuwa ni mkombozi , akiwahakikishia wale aliowadanganya  kuwa ni uwezo wake uliowafufua  kutoka  kutoka makaburini mwao ,shetani  atawafanya waliodhaifu  kuwa na nguvu  na atawavuvia wote  kwa  uwezo wake kuwaongoza  kuutwaa mji wa Mungu ,

IV.            Shambulizi la mwisho dhidi ya Mungu                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                           

Shetani  atashauriana  na watu  hawa wenye  nguvu.watasema kwamba jeshi lililo  ndani ya mji  ni dogo  likilinganishwa na  la kwao na kwamba wataweza kushinda.mafundi wenye ujuzi  watatengeneza zana za vita .viongozi wa kijeshi  watapanga watu  mapenda vita  katika makundi na vikosi

Hatimaye amri ya kusonga mbele  itatolewa  na jeshi  lisilohesabika litasonga mbele ,jeshi hili litakuwa  kubwa kiasi kwamba  muungano  wa majeshi  ya zama zote  hautalingana nalo.shetani ataongoza kikosi cha mstari wa mbele ,wafalme wa mashujaa wake  watakuwa kwenye  msururu wake .kwa umakini wa kijeshi wanajeshi  wakiwa wamejipanga  kwenye mstari kulingana na vyeo vyao .watasonga mbele juu ya uso wa nchi uliobomolewa,,wakiuelekea mji wa Mungu .kwa amri ya  YESu malango ya  Yerusalemu Mpya  yatafungwa na majeshi ya Shetani  yatajipanga tayari  kwa mapambano

  V.            Hukumu yatolewa  dhidi ya  waasi (hapa kila mmoja ataonyeshwa  maisha yake na jinsi alivyomkataa kiristo)

kutawazwa kwa Kiristo kutafanyika  mbele ya mkutano wa wakazi  wa dunia na  wa mbinguni .na sasa  akiwa amevikwa  enzi na nguvu  mfamle wa wafalme atatoa  hukumu kwa waasi ambao waliasi sheria na  mfalme wa wafalme atatoa  hukumu kwa  waasi  ambao waliasi sheria  na  kuwatesa watu wake ufunuo 20:11-12……

Macho ya Yesu  yatakapowaangalia waovu ,wataitambua kila dhambi  ambayo waliwahi kuitenda .wataona ni wapi miguu yao ilitanga pembeni  mbali nanjia takatifui  .majaribu yenye kushawishi ambayo waliyawezesha kwa  kuendekeza dhambi,wajumbe  wa Mungu  waliopuuzwa,maonyo yaliyokataliwa ,mawimbi ya rehema  yaliyorudishwa nyuma  kwa ukaidi,moyo usiotubu yote yataonekana  kana kwamba  yaliandikwa kwa herufi za moto .Juu ya KITI CHA ENZI MSALABA UTAINULIWA. kama kulivyo kuonekana kwa SINEMA,yataonekena  mazingira  ya anguko  la ADAMU  na hatua zilizofuata  za mpango wa ukombozi;(KWA UFAFANUSI ZAIDI SOMA KITABU KILICHOANDIKWA NA ELLEN G WHITE CHA TUMAINI KUU ,SURA YA 42)

Baada ya kila mmoja muovu kujiona jinsi mbingu zilivyoshulikia wokovu wake ili aokolewe lakini akakataa yeye mwenye kila mmoja atakili akisema MUNGU HUKUMU ZAKO NI ZA KWELI NA ZA HAKI  na baada tu ya  tukio la kukili linalofuata ni waovu kuchomwa moto pamoja na SHETANI UFUNUO 20:10 ;

SOMO LINALOFUATA NI UNABII UNAOHUSU MAKANISA SABA.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MIAKA ELFU MOJA YA WATAKATIFU MBINGUNI;S/N 19




JE MBINGUNI NI MAHALI HALISI-JIBU NDIO

YOHANA 14:1-3, Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. WAEBRANIA 11:16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

VITU AU MAMBO YATAYOKUWA YANAENDELEA MINGUNI BAADA YA WAKATIFU KUFIKA

          i.            WAKATIFU WATAKAPOFIKA MBINGUNI WATAKARIBISHWA NA YESU

 Mathayo 25:34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu

       ii.            YESU ATAWAVISHA TAJI YA USHINDI

Watapewa taji ya uzima “thawabu yaani, utukufu ule wa mbinguni, watakaopewa washindi wale, italingana na kiwango walichoweza kuiwakilisha TABIA YA KIRISTO katika Ulimwengu huu..Taji ya Uzima itangaa sana  au itakuwa na mwanga  uliofifia ,itametameta ikiwa  na nyota nyingi,au itaangazwa kwa johari chache sana ,kulingana na mwenendo wetu wenyewe(OHC 123) ,2 WAKORINTHO 9:6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.

     iii.            WATAKATIFU WATAFANYIWA KARAMU KUBWA YENYE VINONO

ISAYA 25:66 Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.

     iv.            KAZI MOJAWAPO WATAKAZOKUWA WANAZIFANYA WATAKATIFU NI KUPITIA HUKUMU AMBAZO YESU AMEKWISHA KUZITOLEA MAAMUZI,HUO NDIO UTAKUWA WAKATI WAKUTAMBUANA KWA NINI FURANI HAKUOKOLEWA

1 WAKORINTHO 6:2-3 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya UFUNUO 20:4-6Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. , (1 WAKORINTHO 4:5)

        v.            WATU WATAKUWA NA MAUMBILE GANI?

Urefu  wa karibu  futi kumi na mbili” wakiwa wemerejeshwa kwenye mti wa uzima  katika edeni ile iliyopotea zamani  sana wale waliokombolewa  wataendelea kukua (malaki 4:2) na kufikia kimo kamili  cha  jamii  ya wanadamu wa asili katika utukufu wake (gw 676) yeye adamu alikuwa na erefu  wa zaidi ya mara  mbili kuliko  ule  wa mwanadamu wanaoishi sasa na mwili wake  uliumbika ukiwa na uwiano mzuri

  vi.            JE MAUMIVU, KIFO YATAKUWAPO?

Maumivu hayawezi kuwako katika mazingira yale ya mbinguni .hapatakuwepo na machozi tena ,wala misafara  ya mazishi ,wala tepe za maombolezo ,wala kilio..kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita ,wala hapana mwenyeji  atakayesema  mimi  mgonjwa ( UFUNUO 21:4,ISAYA 33:24),(GW 676)

   vii.            JE KUMBUKUMBU ZAO ZITAKUWEJE

Kumbukumbu zetu zitakuwa kamili kabisa watu wale  walioishi kabla ya gharika  walikuwa  hawana vitabu  hawakuwa na kumbukumbu zote zilizoandikwa ,lakini wakiwa wenye nguvu  nyingi za kimwili na kiakili ,walikuwa na kumbukumbu zao thabiti ,zenye uwezo wa kunasa kile walichokuwa  wameambiwa ,nao kwa zamu yao  kuweza  kuwapa wazao wao  bila kuuathiri ujumbe ule

viii.            JE MACHO YAO YATAKUWA NA UWEZO GANI?

Watakuwa na macho  kama DARUBINI  yaonayo vitu vidogo sana na vile  vilivyo mbali sana  kwa macho  yaonayo wazi  kabisa  wataangaza na  kuungalia  utukufu wa uumbaji

  ix.            JE UWEZO WAO WA KUSAFIRI UTAKUWAJE?

Uwezo wa kusafili katika anga msongamano wa waliokombolewa utazunguka toka Dunia moja  kwenda Dunia  nyingine na wakati wao mwingi utatumika  katika kuzichunguza siri za ukombozi

       x.            JE KUTAKUWA NA MAISHA YA KIFAMILIA, NDOA NA KUZAA WATOTO KULE?

Hakuna ndoa kule wala kuzaa watoto kuna watu leo wanaoeneza imani yao  wakisema  kwamba kutakuwa  na ndoa  na kuzaa watoto katika nchi mpya ,lakini basi  ,wale wanaoyaamini maandiko  hawawezi kulikubali fundisho  kama hilo ,fundisho linalosema  kwamba  watoto watazaliwa katika nchi mpya  halina sehemu   katika  lile  neno la unabii lililo imara zaidi (MM99,1SM 172) MATHAYO 22:23-30

  xi.            NI KUMBUKUMBU GANI MOJA PEKEE YA KAZI YA KIKATILI ILIYOFANYWA NA DHAMBI AMBAYO ITAKUWA MBELE DAIMA?

Kumbukummbu moja pekee itabaki: mkombozi wetu daima  atachukua  alama  zile za kusulubiwa  kwake . Juu ya kichwa chake  kilichojeruhiwa ,ubavu ni pake ,katika viganja  vyake  vya mikono  na miguu ,hizo ndizo alama pekee za kazi  ya kikatili  ambayo  dhambi  imefanya kwake(gw)

 

  xii.            JE MBINGUNI KUTAKUWA NA IBAADA?-JIBU NDIO

Kukusanyika pamoja kumwabudu Mungu. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na SABATO HATA SABATO, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.

xiii.            JE NI MASOMO YAPI WATAJIFUNZA WATAKATIFU

Baadhi ya masomo wakayojifunza ni haya watajifunza HISTORIA YA PAMBANO KUU ,kugundua SABABU YA MATATIZO YOTE YA MAISHA HAYA  ,KUJIFUNZA USHINDI WA KILA TENDO JEMA NA BAYA  KATIKA MAISHA HAYA  WATATUNGA NYIMBO NA KUSILIZA  MUZIKI ULE ULIO MKAMILIFU SANA na mengineyo

MPENDWA USIKOSE jitahidi ukaone mwenyewe somo linalofuata mji MPYA YERUSALEMU UKISHUKA KUTOKA MBINGUNI usikose.