UFUNUO
6:1 Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo
alipofungua moja ya zile muhuri Saba, nikasikia mmoja WA wale wenye uhai wanne
akisema, Kama Kwa sauti ya ngurumo, Njoo
JE
MUHURI SABA INAWAKILISHA NINI?-MUHURI SABA Inatuleta
ama katika ushindi wenye utukufu au katika kushindwa kunakotisha katika ibaada
ya utukufu ya kuja kwa YESU.
JE
FARASI HUWAKILISHA NINI?- FARASI NI mfano
wa wajumbe wa MUNGU wajumbe waliotumwa kuleta vyote wokovu na
hukumu.
MUHURI
WA KWANZA.(kanisa la Efeso)
FARASI MWEUPE.
UFUNUO
6:2
Nikaona, Na tazama, farasi mweupe, Na yeye aliyempanda
ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda
MAANA
YA KWANZA YA FARASI MWEUPE-Farasi mweupe Ni mfano wa kuhesabiwa haki
na ushindi.
MAANA
YA PILI YA FARASI MWEUPE-Farasi mweupe Ni barabara ya kufaulu injili
katika karne ya kwanza ya historia ya Ukristo, hii ilikuwa mfano wa kanisa la
Mitume sawa na MFANO WA KANISA LA EFESO katika
Ufunuo 2:1
UTA
UNAMAANISHA NINI?-Uta katika mkono ni uhakikisho
wa ROHO
Mtakatifu
katika mioyo ya wanadamu.Maneno ya mitume yalikuwa makali Kama mishale ya
Mwenyezi yakithibitishia wadhambi uovu wa kutisha katika kukataa na kumsubisha
Bwana wa utukufu.
MUHURI
WA PILI (kanisa Smirna)
FARASI
MWEKUNDU.
UFUNUO
6:3-4 Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye
uhai wa pili akisema, Njoo! Akatoka farasi
mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika
nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa
FARASI
MWEKUNDU HUWAKILISHA NINI ?–Ni mfano wa mauaji na mateso waliofanyiwa
wafuasi wa YESU baada ya wakati wa Mitume ambacho ndicho kipindi cha KANISA LA
SMIRNA KATIKA UFUNUO 2:8
MUHURI
WA TATU.(
kanisa la pergamo)
FARASI
MWEUSI
UFUNUO
6:5-6 Na alipoifungua muhuri ya tatu,
nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi
mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti
katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na
vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai
FARASI
MWEUSI ALIWAKILISHA NINI?-Aliwakilisha
hali za watu wa MUNGU zilikuwa zinaendelea kuwa
ngumu kwanza .FARASI MZURI MWEUPE akiwa
mfano wa usafi na ushindi halafu MWEKUNDU sana
ni mfano wa mateso na kisha sasa mfano
wa kutisha wa njaa( farasi huyu MWEUSI
nawakilisha kuwa ne no la Mungu
liliadimika siku hizo za kanisa la
pergamo)
SAUTI
ILIYOTANGAZA HABARI MBAYA kibaba
cha ngano au shayiri kilikuwa ndicho posho ya kila kila siku kama vile ratili
moja na nusu ya unga wa mahindi wakati
mwingine unafikiliwa kilikuwa chakula
cha kila siku cha askari wa kiafrika.RUPIA katika nyakati za agano jipya ilikuwa ndiyo ujira wa kibarua kwa siku nzima
(Mathayo 20:1,20)
PERGAMO
CHA UFUNUO 2:12 Hekaya za kupendeza na mapokeo ya wanadamu yalilisonga mno neno
la Mungu wale waliokwenda kanisani walipata chakula haba cha kulisha roho zao
Nakala
za biblia zikawa adimu kiasi kidogo tu cha neno la MUNGU kikawa na thamani kama
chakula kidogo wakati wa njaa
MUHURI
WA NNE (kanisa la Thiatira)
FARASI
WA RANGI YA KIJIVUJIVU
UFUNUO 6:7-8 Na
alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema,
Njoo! Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda
jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo
ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.
RANGI
YA KIJIVUJIVU HUWAKILISHA NINI?-Rangi hii inaonyesha rangi ya mauti
yenyewe.wanafunzi wa biblia wameelewa
kwa miaka mingi kuwa farasi wa nne maana
ya hali ya UFU YA KANISA la(zama za kati) wakati kati ya mwaka 538 BK mpaka wakati matengenezo
ya Kiprotestanti wakati ambapo kanisa liliokolewa sehemu tu kutoka nguvu za UPAPA.
ROHO YA
NCHI HUWAKILISHA NINI?-Robo ya nchi itakuwa basi na
maana ya sehemu ya nchi ya mateso ya MAMILLIONI YA MASHAIDI WA
WAKATI WA ZAMA ZA GIZA (538 BK-1517 BK)
MUHURI
WA TANO.(kanisa la sardi)
UFUNUO
6:9-11 Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya
madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya
ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu,
Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao
juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu,
nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya
wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao
NGUO
NDEFU HUWAKILISHA NINI?-Kwa kawaida inaeleweka kwamba maneno NGUO
NDEFU
nyeupe huwakilisha heshima Kwa Mashahidi Waliokufa Kama KAFARA
YA UPAPA.
MFANO
WA WATU WALIOVIKWA NGUO NDEFU NYEUPE -Kwa maana ya kwanza watu Kama
WYCLIFFE.HUSS NA JEROME walikuwa wamechukiwa na UPAPA walipewa heshima kuwa
watumishi wa kweli wa Mungu. KIPINDI HIKI KILIANZA
(1517-1798)
MUHURI
WA SITA.(kanisa la Filadelfia)
UFUNUO
6:12-17 Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya
sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa,
mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini
upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu zikaondolewa
kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali
pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu,
na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya
milima,
MUHURI
WA SITA ULIANZA (1798 A.D-1844 A.D)`Nyakati za zama za giza
sasa zimekwisha pita na matukio makubwa yanaanza kutokea duniani .
KULITOKEA
NA MATUKIO KAMA YAFUATAYO MOJA –
TUKIO
LA KWANZA LA TETEMEKO-Tetemeko kuu ambalo halijawahi kutokea mnamo
asubuhi ya Novemba 1, 1755. karibu WATU 30,000
waliuawa katika muda wa DAKIKA SITA.
TUKIO
LA PILI LA GIZA - -Tukio kubwa lilifuatia miaka
michache baadaye siku ya Mei 19, 1780 siku ya kiza.
TUKIO
LA TATU LA KUUNGUKA KWA NYOTA LILIFUATA-Nyota za mbinguni zikaanguka
juu ya nchi Kama vile mti upukutishavyo mapooza yake Novemba 13.1833.
MUHURI
YA SABA. ( kanisa la laodikia)
UFUNUO
8:1 Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni
kama muda wa nusu saa. Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za
Mungu, nao wakapewa baragumu saba. Na malaika mwingine
akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba
mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya
dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
NINI
KINACHOLETA KIMYA HIYO?-sura ya saba imetupwa kati ya sura ya kufungua muhuri ya sita tuliona waovu
wakiiambia miamba na milima
iwaangukie na kuwasitiri mbele za
uso wake
yeye aketiye juu ya kiti cha enzi
na hasira ya mwana kondoo
Mamia
ya wengi wa wakaaji wa Dunia wameukataa msalaba na wamechagua kuangamia
na hivyo wakati wakiangamia kuna kuwa kimya mbinguni
MUDA
HUU WA NUSU SAA HUWALIKISHA NINI?- Nikipindi cha unabii ambacho
siku ni sawa na mwaka mmoja basi kimya kitachukua kama juma moja.